Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) limetoa mifuko 500 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule za secondari zenye uhaba wa madarasa licha ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Arusha.
Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dr. Barnabas Mtokambali amekabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuziba pengo la upungufu wa madarasa,ambapo amesema kuwa kanisa hilo limeaona lishiriki katika maendeleo ya jamii kwa kusaidia ujenzi wa madarasa.
Alisema kuwa kanisa linatambua juhudi zinazofanywa na serikali katika kutoa elimu kwa Watanzania hivyo wameamua kuungana na serikali kwa kutoa mifuko hiyo kama chachu ya maendeleo ya elimu katika mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa kanisa la TAG limekua la kwanza katika kutoa msaada kwa serikali na kuwezesha ujenzi wa madarasa kwani ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa huku madarasa yakiwa machache.
Gambo alisema kuwa serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo wataendelea kushirikiana katika kuwahudumia Watanzania.
“Taasisi za dini ni wadau wakubwa wa maendeleo ambao licha ya miradi ya kuhudumia wananchi bado wanaliombea taifa amani ambayo ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa” Alisema Gambo
Muumini wa Kanisahilo Danford Massawe alisema kuwa makanisa yanapaswa kuiga mfano wa kanisa la TAG katika kushirikiana na serikali katika masuala ya maendeleo ili kuharakisha maendeleo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dr.Barnabas Mtokambali akikabidhi mifuko 500 ya saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika halfa fupi iliyofanyika jana jijini Arusha.Picha na Mahmoud Ahmed Arusha
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments