SOKO la Ilala Boma Jijini Dar es Salaam linaendesha zoezi lakuwasajili wafanyabiashara wote sokoni hapo wanao miliki vizimba na meza nakuwarasimisha katika mfumo wa kanzi data, mfumo huo unatajwa kuwa muoarobani wa kuvamia soko hilo. Mwandishi wa gazeti hili jana alishuhudia wafanyabiashara wakijisajili katika ofisi ya Ofisa Mkuu wa soko, kukamilika kwa kanzi data hiyo kutasaidia soko hilo kutoa huduma stahiki na kwa weledi wa hali ya juu na kusaidia katika tathimini ya ujenzi wa soko jipya. Akizungumza katika soko hilo Ofisa Mkuu wa soko , Seleman Mfinanga alisema Uongozi wa soko pia umedhamiria kuboresha mazingira ya soko hilo kwa kugawa namba kwa ajili ya kuwatambua wafanyabiashara wa soko hilo. Mfinanga alisema Uongozi wa soko hilo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ipo katika mpango wakuboresha masoko yake yote likiwemo la Ilala Bora. Akijibu malalamiko hayo Mfinanga alikiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizoainishwa nakuzitolea ufafanuzi...