Skip to main content

Posts

Katibu Mkuu Kiongozi mpya akaribishwa, atembezwa Ikulu leo

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi akiwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi akikatibishwa Ofisini kwake na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, Ikulu Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, akitembezwa maeneo mbali mbali ya Ikulu Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi akizungumza na Baadhi ya Madereva wa Ikulu, wakati akiwa katika ziara ya kutembelea maeneo mbali mbali ya Ikulu, Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, Ikulu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha Ofisini kwake, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu K...

Mjue mpenzi mpya wa Baraka da Prince

Baada ya kuwa na stori tofauti kusamba kwenye mitandao ya kijamii, imesemekana kuwa kwa sasa msanii wa mziki wa bongo fleva Baraka da Prince hayuko tena na msanii wa filamu Tanzania Nisher ila anatoka na msanii wa bongo Fleva Najma Aka Naj. Haya ni maneno ya Barak Da Prince yaliyoambatana na Post ya kichwa cha mwanamke aliyelala naye.

Majaliwa ampa siku 8 DED kuhama gesti

Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa siku nane kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega, Hamis Yuna, kuhamia kwenye halmashauri hiyo kutokana na kuishi nyumba ya kulala wageni iliyopo wilaya jirani ya Magu. Pia, Majaliwa ametoa siku 13 kwa watumishi wote wanaoishi Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, kuhamia wilaya hapa ifikapo Machi 15. Akihutubia wakazi wa Kata ya Lamadi wilayani hapa jana, Majaliwa alisema hatapenda kumuona mtumishi kufanya kazi akitokea wilaya nyingine ilhali kuna nyumba nyingi za kutosha. Alisema watumishi wanaoshindwa kuishi maeneo yao ya kazi, wanawakosesha huduma wananchi wanaotegemea. Majaliwa alisema haiwezekani mtumishi kuishi wilaya nyingine na kufanya kazi kwingine na kwamba, muda mwingine hufunga mapema ofisi ili kuwahi usafiri. “Nampa siku nane mkurugenzi kuhamia makao makuu ya wilaya hiyo na watumishi wote kufikia tarehe 15 wawe wamehamia hapa, mkuu wa wilaya utaniju...

Conor McGregor anyukwa na Nate Diaz

Conor McGregor alipigwa na Nate Diaz katika raundi ya pili Conor McGregor alipigwa na Nate Diaz kwa kusalimu amri kwenye UFC 196. McGregor alikubali kusalimu amri baada ya kukabwa koo katika raundi ya pili na Diaz mjini Las Vegas. Nate Diaz akishangilia ubingwa baada ya kumpiga McGregor “Nimevunjika moyo. Nitaendelea kusikiliza nani mashabiki wangu wanataka nipigane naye kutetea mkanda wangu,” alisema McGregor. McGregor alisalimu amri baada ya kukabwa koo na Diaz Kwa upande wa wanawake Miesha Tate alimnyuka bingwa Holly Holm kwa kusalimu amri katika raundi ya tano. Miesha Tate akishangilia ubingwa wake dhidi ya Holly Holm Raia wa Ireland Conor McGregor atajiandaa kurudi Octagon kupambana na kati ya Jose Aldo au Frankie Edgar. Holly Holm alisalimu amri baada ya kukabwa koo na Miesha Tate

DC -PAUL MAKONDA AZINDUA VITAMBULISHO VYA WALIMU KUPANDA DALADALA BURE JIJINI DAR

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam jana asubuhi, baada ya kuvizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao. DC Makonda akimfika kitambulisho Mwalimu Gideon Mwenenyi. DC Makonda akimvika kitambulisho, Mwalimu Ramadhani Korowelle. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo. (P.T) Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Turiani, Alpherio Nchimbi (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo. Walimu na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla hiyo Wananchi na walimu wakiwa kwe...

Kutoka Facebook

Pierre Mayombo ‎   to   SPORTS EXTRA Jamie Carragher: "Wachezaji wa Liverpool huwa hawajirushi, Ile ilikuwa penati ya wazi tu!!!" Sasa angalia vizuri hizo picha Benteke alijirusha dhahiri!!!Alipoulizwa akasema jibu lenye kigugumizi!!!eti anaamini aliguswa,asingeguswa asingeanguka!!!

Tottenham v Arsenal dimba la White Hart Lane

Kikosi cha Tottenham Spurs Tottenham itakuwa alama sita juu ya mahasimu wao Arsenal endapo watashinda leo katika dimba la White Hart Lane. Kikosi cha Mauricio Pochettino kitakuwa na nafasi kubwa kutokana na ukweli kwamba mahasimu wao watawakosa Petr Cech na Laurent Koscielny. Delle Alli wa Tottenham Spurs Ushindi huo wa nyumbani utawapaisha Spurs juu kwenye msimamo wa ligi huku vinara Leicester City wakisubiria mechi na Watford. Tottenham iko nyumba alama tatu dhidi ya Leicester City. Matokeo ya mechi tano zilizopita kati ya Spurs na Arsenal Vikosi vya timu hizo ni; Tottenham XI: Lloris; Walker, Alderweireld, Wimmer, Rose; Dembele, Dier; Lamela, Eriksen, Alli; Kane Akiba: Vorm, Davies, Trippier, Carroll, Chadli, Mason, Son Arsenal: Ospina; Bellerin, Mertesacker, Gabriel, Gibbs; Elneny, Coquelin; Ramsey, Ozil, Sanchez; Welbeck Akiba: Macey, Chambers, Monreal, Flamini, Campbell, Walcott, Giroud Msimamo wa Ligi Kuu kabla ya mechi za leo