Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15 baada ya kuichapa Nkana FC ya Zambia.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kufuzu kwa uwiano wa mabao 4-3.
Simba ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki iliyofanikiwa kutinga hatua hiyo, ambapo sasa inaungana na wababe wengine 15, ikivunja rekodi yake iliyoiweka mara ya mwisho mwaka 2003.
Timu zilizofuzu hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika ni:
Simba Sc (Tanzania), Asec Memosas (Ivory Coast), Al Ahly (Misri), AS Vita (Congo DRC), JS Saoura (Algeria), Club Africain (Tunisia), Al Nasri (Libya), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), FC Platinum (Zimbabwe), CS Constatine (Algeria), TP Mazembe (Congo DRC), Orlando pirates (Afrika Kusini), Lobi Stars FC (Nigeria), Wydad AC (Morocco), Ismaily SC (Misri), Horoya SC (Guinea).
Droo ya hatua hiyo ya makundi inatarajia kufanyika Desemba 28 mwaka huu.
Comments