Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesmea kuwa hana hofu na mchezo wake wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya Nkana FC ya Zambia kwa kuwa kikosi chake ni moto wa kuotea mbali.
Simba watacheza na Nkana FC Desemba 15 ikiwa ni hatua ya kwanza baada ya kuvuka hatua ya awali kibabe kwa kuwapiga Mbabane Swallows ya Eswatin mabao 8-1.
"Tupo vizuri kuelekea katika mchezo wetu dhidi ya Nkana FC, kikubwa tunachohitaji ni ushindi ili kuongeza kujiamini kwa wachezaji wangu, kila kitu kitakuwa sawa kwa kuwa wapinzani nawatambua," alisema.
Simba wanatarajiwa kukwea pipa kesho kuwafuata Nkana FC ya Zambia ambayo Mtanzania Hassan Kessy anacheza na mchezo wa marudio unatarajiwa kuwa Desemba 23 uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Comments