KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel Tanzania,imeingia katika makubaliano rasminna kampuni ya michezo ya kubahatisha na kubashiri ya Biko Tanzania ilikuongeza msisimko na ushirikiano kwa wadau wa michezo hiyo nchini katika msimu huu wa siku kuu.
Ushirikiano huo utawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Halotel
kupitia huduma ya kifedha ya Halo Pesa kupata fursa ya kuvuna
mamilioni kutoka Biko Tanzania kwa kubahatisha na pia kubashiri
matokeo ya michezo mbali mbali na Bikosports.
Akizungumza na waandhishi wa habari makao Makuu ya Ofisi za Halotel
Dar es Salaamleo , Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel,Mhina
Semwenda amsema, ushirikiano huo baina ya kampuni yao na Biko unaweze
sha wateja wao kuweza kushiriki na kupata fursa ya kujishindia fedha
zitakazowezesha kujiongezea kipato na hivyo kuboresha maisha yao.
"Mtandao wetu na huduma ya Halopesa imeenea nchini nzima katika maeneo ya mjini na vijijini,jambo ambalosasa litatoa fursa mpya ya ushiriki
michezo kwa watejas wetun walioko nchi nzima,ambao kwa namna moja ama
nyingine walikuwa hawapati fursa hii ya kushiriki,tunaamini sasa wateja
wetu walioko nchi nzima w3ataweza kushiriki katika michezo ya kubashiri na kubahatisha kupitia Biko Tanzania,"Amesema Semwenda.
Semwenda amesema hiyo ni fursa kwa wateja wate wa Halotel mijini na
vijijini kuweza kushiriki katika michezo ya kubahatisha na kubashiri kama vile mpira wa miguu,mpira wa kikapu,Rugby,Cricket,Tennis na
mingiuneyo ambapo hapo kabla hawakuweza kupata fursa kushiriki katika
michezo hiyo kwa kupitia mtandao wa Halotel(HaloPesa) kwa kutumia namba
USSD za Halopesa ambazo ni (*150*88#)wenye mawakala zaidi ya elfu 55,000.
Kampuni ya Halotel imesema kuwa wateja wao wanatakiwa kufanya miamala
kwenye simu za mkononi ambapo namba ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456 au sawa na neno biko kwa kupiga namba *150*88#,kuchagua lipa
bili na Halopesa,kisha chagua 4:Michezo ya kubahatisha ambapo namba
5 ni Biko(505050)kisha namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456,kisha ataweka
kiasi pamoja na namba ya siri kukamilisha muamala.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven amesema hiyo ni
nafasi ya muhimu kwao na kwa wateja wa kampuni ya simu ya Mkononi ya
Halotel Tanzania kwa kupitia huduma yao HaloPesa.
"Kama mnavyojua ,Biko ni kampuni kubwa na madhubuti inayojihusisha na
michezo ya kubahatisha kwa kufanya miamala kwenye simu za mkononi ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456 au sawa na neno biko mbali na hilo,pia tunaendesha mchezo wa kubashiri matokeo ya
michezo mbali mbali duniani ujulikanao kama bikosports,"alieoneza kusema.
Kampuni ya Biko ilinza mapema mwaka jana na imekuwa ikihusisha watu wenye umri kunzia miaka 18 na kuendelea.
Comments