Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wamekubali kupokea kichapo cha magoli 2 – 1 dhidi ya Nkana FC ya Zambia kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Katika kipindi cha kwanza Simba imeonekana ikishindwa kufika langoni mwa timu pinzani na kulazimishwa kurudi nyuma huku viungo wake wakionekana kushindwa kufanya vizuri.
Mabao ya Nkana yamefungwa na Ronald Kampamba dakika ya 27 huku la pili likifungwa na Kelvin Kampamba dakika 56 huku Simba wakipata bao lao kupitia kwa nahodha John Bocco kupitia mkwaju wa penati baada ya Meddie Kagere kufanyiwa madhambi.
Simba sasa italazimika kufunga goli moja kwa bila kama inahitaji kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika.
Wawakilishi wengine wa Tanzania, Mtibwa Sugar hii leo wamekubali kipigo cha mabao 3 – 0 kutoka kwa KCCA mchezo wa kombe la Shiriokisho Afrika uliyopigwa Uganda.
Comments