Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Disemba 14 2018 kimeandaa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005,tuzo hizo zimejikita katika kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wanguvu kazi na rasilimali watu kwa lengo la kuwawezesha kutimiza wajibu wao kikamilifu na kupelekea kukuza uzalishaji wa kibiashara.
Tuzo hizo zilihudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo Mh. Jenista Mhagama, Mh. Anthony Mavunde, Mhe. Stella Ikupa, Mkuu wa MkoaDSM, Mhe. Paul Makonda, Balozi
wa Norway nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Denmark nchini, Bw. Einer H.
Jensen na Balozi wa China nchini Nd. Wang Fe, pamoja na taasisi mbali mbali
ikiwemo TUKTA na ILO.
Tuzo hizo zinazofanyika kila mwaka zimasaidia kuhamasisha wanachama kuchukulia masuala
ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama misingi muhimu katika kumwezesha mwajiri kuwa
na wafanyakazi wenye uwezo na ueledi ili kukidhi mahitaji ya ushindani katika biashara.
Pichani Sherehe ya utoaji tuzo iliyohudhuriwa na Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana.
Sherehe ya utoaji tuzo iliyohudhuriwa na Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, VijanaAjira na Wenye Ulemavu akiwa Mgeni Rasmi, zimekuwa maarufu hapa nchini katika muktadha wa biashara hasa kwa kuhamamasisha makampuni makubwa na madogo na ya ukubwa wa kati
kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora yakufanya biashara nchini.
Tuzo hizo ambazo kwa mwaka 2017 ziliboreshwa kwa kuongezewa vipengele 12 vipya vya Hali
nzuri kwa Wafanyakazi (Employee Wellness),Kuvutia na kutunza wafanyakazi wenye ujuzi
(Attraction and Retention), Mahusiano Mazuri Mahali pa Kazi (Industrial Relations), Kujali kazi na
maisha nje ya Kazi (Work Life Balance), Mwajiri anayekubalika na Kufahamika (Employer
Branding),Usimamizi wa Wafanyakazi kwa kuzingatia Umri (Managing an Aging Workforce).
Uwekezaji katika Teknolojia (Technology Investment), Tuzo kwa ajili ya Sekta Binafsi (Private
Sector Award), Tuzo kwa Sekta ya Umma (Public Sector Award), Tuzo kwa Ajili ya Mashirika ya
Kijamii ( Civil Society Award) na Tuzo ya Mwajiri Mzawa (Indigenous Employer Award) ,
zitaendelea na vipengele hivyo vipya kwani vinatoa fursa kwa wanachama kufanyia kazi vipengele hivyo kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi na ajira kulingana na mahitaji ya waajiri nchini.
Akizumgumza na wageni waalikwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu alisema kwamba serikali inatambua mchango wa waajiri kutoka sekta zote na itaendelea kushirikiana nao pamoja na Vyama vya Wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika kutimiza azma ya nchi yetu
kujitegemea.
Mhe. Jenista Mhagama aliongeza kuwa serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania, Dr. John Joseph Magufuli imebeba jukumu la kuboresha
miundombinu katika nyanja za usafirishaji wa anga, reli na maji, afya, nishati, elimu na
mawasiliano ambayo kwa kiasi kikubwa zinaongeza uzalishaji wa nchi kupitia waajiri wa sekta
binafsi na umma.
Aidha Mh. Mhagama alipongea Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa shughuli zake mbali
ikiwemo Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Uongozi kwa Mwaka
2018, Mwanamke wa Wakati Ujao inayofanyika kwa ushirikiano na Shirikisho la Vyama vya
Waajiri nchini Norway (NHO) kutoa mafunzo kwa wanawake ili waweze kushika za juu za
uongozi katika makampuni na taasisi mbali mbali ambapo tangu kuasisiwa kwake mwaka 2016,
wanawake 66 wamehitimu mafunzo hayo.
Akiongea na wageni waalikwa, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jayne
Nyimbo Taylor alishukuru serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zake katika kuboresha
mazingira ya kufanya biashara nchini kama punguzo la tozo inayolipwa na waajiri kwa ajili ya
kukuza ujuzi mahali pa kazi maarufu kama “Skills Development Levy (SDL)” kutoka 6% mpaka
kufikia 4.5% huku akiiomba serikali kuipunguza tozo hiyo hadi kufikia 2%.
Pamoja na mapendekezo hayo, Bi. Jayne Nyimbo pia aligusia changamoto mbali mbali zinazowakabili waajiri kama ufuatiliaji wa vibali vya kufanya kazi nchini, utaratibu wa malipo yaMfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo sekta binafsi wanalipa 1% huku waajiri wa umma wanalipa 0.5% ya mshahara anaolipwa mfanyakazi, aina mikataba ya ajira pamoja na tozo na faini zinazotozwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).
Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania(ATE), Dkt.Aggrey K. Mlimuka, alitoa shukrani zake za dhati kwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, wageni waalikwa na wadau mbali mbali waliofanikisha Tuzo ya Mwajiri wa Mwaka 2018.
“Naomba nikushukuru tena Mhe. Mgeni Rasmi,na Washiriki wote kwa kuja kujumuika na sisi katika utoaji
wa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018, na naamini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa kushikiana na
TUCTA pamoja na Serikali hasa tunapoendelea kujenga nchi yetu kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Naomba kutumia fursa hii pia kuwashukuru nakuwapongeza wanachama wote walioshiriki katika zoezi hili hasa kwa kujaza dodoso ili kupata fursa ya kulinganisha utendaji wa makampuni yao na ya wengine.” Alisema Dkt. Mlimuka.
“Naomba kuhitimisha salamu zangu kwa kuwatambua uwepo wa baadhi ya wanachama na
wadau wetu kwa michango yao ambayo imetuwezesha kufanikisha utoaji wa tuzo hii ambao ni
wafuatao.” Alimalizia Dkt. Mlimuka.
Kuhusu Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ni chombo pekee cha waajiri kinachowawakilisha vema nchini Tanzania. Kiliundwa mwaka 1960 ili kusimamia na kulinda maslahi ya waajiri katikamasuala ya kazi na ajira.
Kama sauti muhimu ya masuala ya kibiashara, Chama cha waajiri Tanzania kinawakilisha waajiri
katika sekta zote zinazohusu uchumi wa taifa isipokuwa zile za utumishi wa umma.
ATE ina jumla ya wanachama wa moja kwa moja wapatao 1500 waliosajiliwa na wengine zaidi ya 6000
wasio wa moja kwa moja wanaaotoka makampuni binafsi ya kibiashara na baadhi ya mashirika
ya umma.
Aidha zaidi ya mamlaka yake kuu ya kulinda maslahi ya waajiri na kuhakikisha mahusiano
mazuri baina ya waajiri na waajiriwa makazini, Chama cha Waajiri Tanzania pia kinahamasisha
na kuchochea mienendo mizuri ya usimamizi wa rasilimali watu na misingi bora miongoni mwa
waajiri ili kurahisisha uendeshaji wa biashara ambao ni muhimu katika uzalishaji na ushindani na
hivyo huandaa tuzo za waajiri kila mwaka ili kutambua na kuthamini makampuni yaliyofanya
vema katika kulinda misingi na mienendo ya usimamizi wa rasilimali watu.
Chama hutoa uanachama unaojumuisha makampuni makubwa, ya kati, madogo na madogo zaidi kutoka sekta mbalimbali za uchumi wa taifa.
Wanachama ni pamoja na makampuni binafsina ya umma,mashirika ya umma, vyama vya ushirika, balozi mbalimbali, vyama vya kibiashara,taasisi za kidini, asasi binafsi (NGOs), na watu binafsi. Uanachama wa ATE upo kwa ajili ya waajiri wote nchini Tanznia:- watu binafsi,vikundi, makampuni, mashirika ya umma, serikali za mitaa na mamlaka zingine za nchi au vyama vya waajiri na kwa sasa chama kimegawanyika katika idara 8 ikiwemo kilimo, biashara, viwanda, ushirika na huduma, benki na fedha, madini, mafuta na
usalama binafsi.
Comments