Serikali imesema utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka (Hoima) Uganda hadi Mkoani Tanga haujasimama na kwamba hatua za utekelezaji wa mradi huo zinaendelea .
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani baada ya kumalizika Mkutano wa majadiliano ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba hilo uliomkutanisha na Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni.
Amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo uko katika hatua nzuri na kwamba pande zote mbili wamejadiliana na kukubaliana kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa pamoja na hatua za utkelezaji za mradi.
“ Mradi haujasimama tunaendelea na utekelezaji tumekubaliana tukamilishe ndani ya waakati tuliokubaliana pande zote mbili,” amesema Dkt. Kalemani.
Amebainisha kuwa katika upande wa Tanzania tayari wamekamilisha tafiti ya tathmini ya mazingira, ustawi wa jamii pamoja ulipaji fidia mkoani Tanga.
Dkt. Kalemani amesema malengo ya majadiliano ya mkuano huo ni hatua za utekelezaji wake ikiwemo usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na kuyauza nje za nje.
Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa manufaa kwa jamii na makampuni ya ndani na kusisitiza bomba lina urefu kilometa 1435 huku kilometa 1115 zikiwa sehemu ya Tanzania.
Kwa upande Waziri Muloni amesema watahakikisha watafikia makubaliano na makampuni ili yaweze kusaini utekekezaji wa mradi ukamilike mwaka 2020 ilivyopangwa.
Amefafanua kuwa ifikapo Januari 14 mwakani mkutano mwingine utafanyika nchini Uganda lengo likiwa kujadiliana mambo yaliyobaki makampuni yaanze utekelezaji.
Comments