MAMLAKA ya chakula na dawa (TFDA), imefanikiwa kufikia
na kuvuka malengo iliyojiwekea katika udhibiti wa ubora, usalama na
ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendendanishi ili
kulinda afya ya jamii.
TFDA
imeweka mifumo na taratibu za ndani za utoaji huduma bora kwa
kuzingatia viwango vya kimataifa vya ISO 9001:2015 kwa huduma za kawaida
na ISO 17025:2005 kwa huduma za maabara.
Hayo
yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA
Adam Mitangu wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi za udhibiti wa
ubora,usalama na ufanisi wa bidhaa chini ya serikali ya awamu ya tano.
Alisema
kuwa,mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka
ambapo idadi ya bidhaa za chakula,dawa, vipodozi,vifaa tiba na
vitendanishi imekua ikiongezeka mwaka hadi mwaka,katika kipindi cha
2015/2016 hadi17/18.
''TFDA
imesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa
zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 62,
ambapo imetokana na kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni
mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara,''alisema Fimbo.
Alisema
TFDA imeweka mifumo ya utoaji wa huduma kwa kutumia teknolojia ya
habari na mawasiliano (TEHAMA) ambapo taarifa na takwimu TFDA zikiwemo
za bidhaa na majengo yaliyosajiliwa na zile za wateja zimewekwa katika
mfumo maalumu uitwao IMIS.
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa, mfumo wa IMIS kwa kiasi kikubwa umerahisisha
utoaji huduma kwa wateja na kwa sasa wateja wanaweza kuleta maombi yao
kwa mtandao bila kufika ofisi zao.
TFDA
imeeleza kuwa mifumo mingine ambayo imewekwa na mamlaka hiyo ni pamoja
na usimamizi wa rasilimali watu (HR-MIS), uhasibu (EPICOR) pamoja na
mahudhurio kazini na mfumo wa usimamizi wa taarifa za uchunguzi wa
maabara(LIMS).
''Ukuaji
wa viwanda vya ndani na uwezeshaji wa wasindikaji wa chakula katika
jitihada za kujenga Tanzania ya viwanda ifikapo 2025, TFDA imekua mstari
wa mbele katika kutoa msaada wa kiufundi na kuwajengea uwezo wenye
viwanda vya dawa nchini na kushawishi wawekezaji kujenga viwanda vya
dawa,''alisema Fimbo.
Vile
vile kuhusiana na sampuli katika maabala ya TFDA imekuwa na jukumu la
kufanya uchunguzi wa sampuli za chakula kwa lengo la kujiridhisha na
ubora na usalama wake kabla ya kufanya maamuzi ya kiudhibiti ndani ya
mamlaka hiyo.
Comments