Skip to main content

Rais Magufuli Atoa Maagizo Mazito

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania haifanyi vizuri kwenye suala la ukusanyaji wa mapato ukilinganisha na baadhi ya nchi barani Afrika kulingana na pato lake la taifa.
 
Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Tanzania ndiyo nchi yenye wastani mdogo wa kukusanya kodi , ambapo inakusanya asilimia 12 ya kodi huku ikiwa na jumla ya walipa kodi milioni 2 kati ya watanzania milioni 54. Taifa la Afrika Kusini ambalo lina watu milioni 56, wastani wake wa ukusanyaji wa kodi  ni asilimia 26.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akizungumza na TRA na Wakuu wa Mikoa nchi nzima katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam

Rais Magufuli ameiagiza TRA na Wizara ya Fedha kutoza kodi ya nyumba ya TZS 10,000 kwa nyumba za kawaida, TZS 20,000 nyumba za ghorofa zilizopo wilayani na vijijini na Sh 50,000 kwa nyumba kubwa. Tozo hizo zizingatie hati ya kiwanja na sio idadi ya nyumba kwenye kiwanja.

“Katika makadirio ya kodi ya nyumba, wapo wanaokadiriwa hadi Sh. Milioni 2 au Sh. Milioni 3. Nyinyi wakuu wa Mikoa ni mashahidi, mtu amejenga nyumba kwa gharama halafu mnatoza kodi hizo, halafu hata bomba la maji hamjaleta.

“Watanzania tuko Milioni 55 lakini idadi ya nyumba zinazolipiwa kodi ziwe Milioni 1.9. Natoa wito kwa TRA na mamlaka nyingine za mapato hakikisheni mnatengeneza mifumo rahisi kwa wawekezaji na mpunguze vikwazo.

“TRA tumeshindwa hata kurasimisha Sekta ambayo si rasmi ambayo ni asilimia 70, tunakusanya kwenye Sekta rasmi ambayo ni asilimia 30 pekee, tunashindwa kukusanya mapato kwenye Sekta isiyo rasmi, niseme ukweli hatufanyi vizuri kabisa.

“Yapo matatizo katika TRA yenyewe, kwenye mgawanyo wa watendaji katika maeneo mbalimbali. Kuna baadhi ya wafanyakazi wanapigwa vita, wanaondolewa na kuwekwa wengine kwa upendeleo. Lipo tatizo la kubambikizia watu kodi kupitia mfumo wa kukadiria. Mtu ana biashara ndogo anakadiriwa kodi kubwa, mwisho wake anafunga biashara, sasa hapo TRA mmepata faida au hasara? Wengine wanafunga biashara na kwenda kufungua upya maeneo mengine.

“Mazingira ya kufanyia biashara nchini bado ni tatizo. Usafirishaji, utitiri wa taasisi za usimamizi na tozo, ucheleweshaji bandarini, tatizo la umeme, kutumia muda mrefu kupata vibali vya biashara. Hatufanyi vizuri katika kuvutia wawekezaji.

“Askari anaweza kujisikia tu kusimamisha gari hata kwa zaidi ya saa 6 kisha ndiyo akaliachia bila kujali kuwa hao ni wafanya biashara na wanajisikia vibaya, mara nyingi hili linafanywa na jeshi la polisi. Nawataka TPA, TRA, polisi na Idara ya uhamiaji mjirekebishe, vipo vitendo vingi vya kukwamisha wawekezaji naomba mlifanyie kazi,” amesema Rais Magufuli.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...