Wazazi wametakiwa kuacha kuegemea kuchangia sherehe za harusi badala yake wajikite kutoa msaada wa kiuchumi kwa watoto
Jamii imeshauriwa kuacha utamaduni wa kuyakimbia majukumu ya malezi ya kiuchumi badala yake
ijikite katika kutoa eliumu ya ujasiriamali kwa watoto itakayosaidia kuwakomboa kiuchumi
pamoja na kuliingizia taifa kipato.
Wazazi wametakiwa kuacha kuegemea kuchangia sherehe za harusi badala yake wajikite
kutoa msaada wa kiuchumi kwa watoto wao wanaoshiriki harusi hizo kuwakwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph
Kakunda katika Maonesho ya Ujasiriamali kwa vijana yaliyoandaliwa na Taasisi ya Nama
inayojishughulisha na masuala ya utoaji elimu ya ujasiriamali kwa vijana na kuwawezesha
kupitia mikopo nafuu.
Amesema kuwa kuna utamaduni umejenga katika jamii ambapo wazazi hutumia fedha nyingi
kwenye sherehe za harusi za watoto na kwamba baada ya harusi wanandoa huishi magumu
kutokana kutowezeshwa kiuchumi.
" Jamii isikimbie malezi ya kiuchumi kwa watoto tuwape elimu ya ujasiriamali tusiishie
katika kuchangia harusi baada ya harusi tukawaacha watoto kwenye hali ngumu," amesema
waziri Kakunda.
Amebainisha kuwa vijana wamekuwa wakishindwa fursa za mikopo sababu ya kutopewa elimu
sahihi ya njia za kupitia na kusisitiza wakati wengine hukwamishwa na watu wasiohusika
nadni ya taasisi husika.
Amesisitiza kuwa tayari ameshaiagiza Sido kutangaza fursa walizonazo ili vijana na watu
wenye nia ya kupata mikopo wachangamkie fursa hiyo na kwa kila wilaya imetengwa sh
bilioni 8 za mikopo kwa wahitaji
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Musa Msingwa amesema hadi sasa wameshawafikia
vijana 130 ambao wamepewa elimu ya kutambua na kuchangamkia fursa zilizopo.
Amefafanua kuwa wana mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanawafikia vijana wengine katika
mikoa mingine ukiwemo mkoa wa Mtwara.
Naye mshiriki wa maonesho hayo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Matatu
Enterprises, Hussein Abeid ameiomba Serikali kuendelea kutoa mitaji kwa wajasiriamali
waweze kutafuta masoko ya uhakika na kujitangaza.
Comments