TIC yampongeza JPM kuionya TRA kuacha Uonevu wa Ukusanyaji na ukadiriaji viwango vya kodi wafanyabiashara na wawekezaji
Kituo
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa
tamko linaoitaka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kutoza na kufanya ukadiriaji wa
makusanyo ya kodi bila uonevu na kuiagiza kutenda haki na kufuata taratibu ili
kuendelea kuwavutia na kuwatengezea mazingira rafiki wawekezaji wa ndani nje
kuendelea kuwekeza nchini.
TIC
imesema tamko la onyo hilo litasaidia
wawekezaji wa ndani na nje kuamini Serikali ya Awamu ya Tano haina ukandimizi
kwao bali ina dhamira ya dhati kuwakaribisha kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Pongezi
hizo zimekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kuionya mamlaka hiyo akiwa kwenye
ziara ya Uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi la Mradi wa Maji
wilayani Arumeru mjini Arusha ambapo aliwaonya baadhi ya watendaji
kuachakuwakadiria wafanyabiashara viwango vikubwa vya kodi hali inayowafanya
wakwepe kulipa.
Pongezi
hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC,
Geoffrey Mwambe katika Kongamano lililowakutanisha wawekezaji wa ndani na
kutoka China ambapo limejadili ushirikiano wa uwekezaji na kibiashara baina ya
nchi hizo.
Amesema
kuwa tamko hilo litasaidia wawekezaji wengi kuchangamkia fursa za uwekezaji
zililopo nchini huku na kusisitiza hata wafanyabiashara
wamelipokea kwa furaha kwani litawaondolea adha na kuwakatisha tama
ya kufunga biashara zao.
“
Tunafurahi na tumelipokea tamko la Rais Magufuli kwa TRA litatengeneza
mahausiano mema kati ya wafanyabiashara, wawekezaji na
Serikali itafungua fursa za uwekezaji nchini,” amesema.
Amebainisha
kuwa tamko la kuitaka TRA kuweka utaratibu mzuri wa wawekezaji na
wafanyabiashara kufanya malipo ya kodi utasaidia kuliongeza taifa mapato
yatakayochangia maendeleo ya nchi.
Amefafanua
kuwa China ni nchi inayoongoza kwa miradi ya uwekezaji nchini ambapo ipo
takribani 723 ambayo imeachangia ajira 84,000 na kwamba TIC itaendelea
kushirikiana na wawekezaji kutoka nchi hiyo.
Kwa
upande wake, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema ni
muhimu kuwakaribisha wawekezaji hao kuwekeza kwenye viwanda vya mazao kwani
kutasaidia kuyapandisha hadhi mazao yetu na kuuza nje.
Waziri
Kakunda amesema uwekezaji wa viwanda hivyo utapunguza uagizaji wa bidhaa nje na
kulipatia taifa fedha za kigeni na kwamba nchi hiyo ina mtaji wa uwekezaji wa
Sh bilioni 5.8 za Kimarekani.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (tpsf), Godfrey
Simbeye amebainisha kuwa taasisi itaendelea kushirikiana na
wawekezaji wa ndani na nje ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 nchi inafikia
uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda.
Katika
hatua nyingine amempongeza Rais Magufuli kwa kuikemea TRA na kusisitiza onyo
hilo litapunguza unyayasaji na kwamba tayari taasisi hiyo imeanzisha dawati la
kuwasiliana na wawekezaji kutoka China.
Balozi
wa China nchini, Wang Ke amesema kongamano hilo litasaidia kutengeneza
mazingira rafiki kwa wawekezaji wa China kuja kuwekeza huku akikazia tayari nchi
imeshariki katika miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa Uwanja wa Taifa,
Maabara ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mwenyekiti
wa Baraza la Uwezeshaji, Uendelezaji Ushirikiano wa Nchi za Kusini na Kusisni,
Lyu Xinhua amesema kutokana mazingira ya uwekezaji kuwa mazuri anaamini
waekezaji wengi watachangmkia fursa za uwekezaji.
Comments