Naibu Waziri wa Fedha na Mpango Dkt. Ashatu Kijaji aibua jambo mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM
Tanzania katika kuandaa rasimali watu iko chini ya asilimia 62 ya viwango vya Dunia ambapo Tanzania imefikia asilimia 53 kufikia huko kumetokana na watu kukosa ubunifu na ujuzi.
Ambapo katika viwango na ujuzi na ubunifu kwa viwango vilivyowekwa ni asilimia 50 ambapo Tanzania imefikia asilimia 40 hivyo wasomi lazima kuondoa hali hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mpango Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji wakati wa mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kila mwaka kuna wahitimu wengi ambao wanaingia katika soko la ajira lakini hakuna matokeo ya kazi wanazozifanya.
Amesema kuwa mikopo Chechefu kupanda kwake kumetokana na wataalam wa fedha ambapo wamepandisha kutoka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 10 na kuendelea.
"Mikopo Chechefu kupanda hakujanywa na mashine bali ni sisi wenyewe ni kazi kwetu wa wataalam wa fedha kutafakari katika kusaidia maendeleo ya Taifa"amesema Dkt.Kijaji.
Hata hivyo amekipongeza Chuo hicho katika ujenzi wa Chuo makao makuu jijini Dodoma na kutaka wajenge kwa kutumia wabia na sio serikali kutoa fedha. Nae Mkuu wa Chuo hicho Profesa Tadeo Satta amesema kuwa cho kina changamoto ya walimu pamoja na kuwa na eneo dogo.
Amesema kuwa wanatarajia kujenga Chuo cha Biashara katika eneo la Nara jijini Dodoma katika kuwasogezea huduma wafanyakazi wa serikali.
Aidha amesema kuwa Chuo kimeendelea kuwa na ushirikiano na wadau katika utaoaji wa elimu bora.
.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akitoa taarifa ya Chuo katika mahafali 44 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika mahafali ya 44 ya Chuo hicho wakiwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM wakiwa katika mahafali ya 44 yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Comments