Wahitimu 1,387 walitunukiwa shahada mbalimbali zitolewazo na
Taasisi ya Ustawi wa Jamii huku idadi ya wanaweke wahitimu ikiipiku idadi ya
wanaume wahitimu katika Taasis hiyo ambapo wanawake ni asilimia 67 na wanaume
asilimia 33.
Taasisi hiyo imetakiwa kuendelea kufanya tafiti
mbalimbali zitazotoa suluhisho za changamoto zinazo likabili Taifa.
Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto ,Idara kuu ya maendeleo ya
jamii Dk. John Jingu wakati wa mahafali ya 42 ya Taasis ya Ustawi wa Jamii.
“Pamoja na changamoto mbalimbali mlizonazo msiache kufanya
tafiti na kubuni kozi zitakazo toa ufumbuzi wa changamoto za wananchi hususani
katika kozi ya Ustawi wa jamii zipo fursa nyingi,”alisema
Vilevile Dk. Jingu alisema changamoto za chuo hicho
zinafanyiwa kazi nakutoa marejeo ya hotuba ya Waziri mwenye zamana ya Wizara
hiyo, Ummy Mwalimu katika mchango wake bungeni wakati alipokuwa akichangia
makadirio ya bajeti 2018/19.
Aidha Dk.Jingu aliwapongeza wahitimu kwakufanya vizuri na
kuwahakikishia kuwa ajira zipo njenje kutokana na stadi na ujuzi waliupata
katika Taasis hiyo mahiri katika masuala ya ustawi wa jamii ikiwemo kujiajiri
na kuajiri wengine endapo watautumia ujuzi walioupata kwa usahihi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Taasis Sophia Simba
aliwataka kushiriki kikamilifu katika mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii
kwakuwa wanaulewa wakutosha wakawaelimishe wananchi kuunga Mkono juhudi za Rais
Dk.John Pombe Magufuli.
“Pasina shaka mnastahili kutunukiwa shahada mnazotunikiwa
lakini mkawe mabalozi wazuri katika mapinduzi ya uchumi hususani uchumi wa
viwanda na uchumi wakati kama Rais wetu alivyofungua njia,”alisema
Makamu Mkuu wa Taasis hiyo Dk.Zena Mabeyo alisema pamoja na
changamoto nyingi zinazo ikabili Taasi, kubwa rasilimali fedha hivyo ameiomba
serikali kuipatia Taasis hiyo fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mipango yake ya
maendeleo.
Miongoni mwa changamoto ni fedha za kufanyia tafiti,
kupandisha wahadhiri madaraja, ununuzi wa vifaa vya kufundishia hususani vya
Tehama, ufinyu wa madarasa, uhaba wa wataalamu hadi kufikia hatua ya kukodi
kutoa Taasis nyingine.
“Pamoja na ukwasi tulionao hatujashindwa kutekeleza majukumu
yetu kwa asilimia kadhaa kulingana na kile kidogo tulicho nacho lakini kuna
kila sababu kuijengea uwezo Taasis hii muhimu katika ustawi wa Taifa na watu
wake,”alisema.
Comments