SERIKALI kupitia kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda imewakaribisha wafanyabiashara kununua korosho na kuzibangua. Mbali na uamuzi huo , Waziri Kakunda amesema Serikali bado inaendelea kuingia mikataba na wabanguaji ili kupunguza mzigo wa korosho. Kakunda ametoa kauli hiyo wakati taarifa ya timu ya pamoja ya wataalamu kuhusu hali ya utekelezaji wa operesheni korosho iliyotolewa Novemba 27 ikionyesha kuwa itachukua muda mrefu kubangua korosho za msimu huu. Novemba 12, Rais John Magufuli alitangaza Serikali kununua korosho yote kutoka kwa wakulima msimu huu kwa bei ya Sh3,300 kwa kilo. Licha ya Waziri Kakunda kusema haina shida kwa ubanguaji kuchukua muda mrefu, amewataka wafanyabiashara wanaoweza kubangua wenyewe wakae meza moja na Serikali ili wauziwe korosho. “Kama mtu anatokea popote iwe ndani au nje akasema mimi nataka ninunue korosho nikabangue mwenyewe, labda ana bei nzuri a...