Mkurugenzi wa TIC Geoffrey Mwambe (wa kwanza kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza Kulia) katika kikao cha kumuaga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama JacksoN Masaka.
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki,Taasisi sekta binafsi Tanzania TPSF na
Ubalozi wa Tanzania nchini Chinaiimeandaa kongamano maalum la kuhamasisha
na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na China katika kongamano
hilo linatarajiwa kufanyika Oktoba 16 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkrugenzi wa TIC Geoffrey I.M
wambe alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kutangaza fursa za biashara na uwekezaji
zilizopo hapa nchini kwa wawekezaji na wafanya biashara wa China fursa ambazo zipo
katika sekta mbali mbali kama vile viwanda ,Madini ,Nishati,Usafiri,Mafuta na pamoja
na Miundombinu.
Alisema sekta zingine ni ujenzi ,uvuvi wa kina kirefu,Kilimo na usindikaji wa
mazao,Afya,Teknolojia ya habari na mawasiliano,Madawa.
"China mpaka Mei mwaka huu inaongoza kwa uwekezaji nchini kwa thamani ya
miradi na tunatarajiwa kongamano hilikuhudhuriwa na wawekezaji wa makampuni
makubwa zaidi ya 100 kutoka China.
Geoffrey alisema China itasaidia kuiweka na kuitangaza Tanzania kama miongoni
mwa maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kibiashara kwa kampuni za kutoka
China.
Aidha alisema makampuni ya kitanzania yanakaribishwa kushiriki kwenye kongamano
hilo ili kuweza kuanzisha , kukuza na kuendeleza ushirikiano katika nyanja za biashara
na uwekezaji kwa kushirikiana na kampni za wafanya biashara wa China.
"Tunategemea Tanzania ita ongeza thamani ya mitaji ya uwekezaji kutoka nje yaani
FDI iwapo makampuni ya China yatakayohudhuria kongamano yata amua kufanya uwekezaji
nchini,"alisema Geoffrey.
Alisema TIC inapenda kutumia fursa hiyo kuitangaza Tanzania kwa ujumla kwani
mpaka sasa mwezi Mei mwaka huu kituo cha uwekezaji TIC,kimeweza kusajili miradi
670 ambayo yenye umiliki wa china inayotarajia kuzalisha ajra zipatazo 83,394 yenye
thamani ya mtaji wa kiasi cha dola za Marekani 5,779 hivyo hiyo ni fursa muhimu kabisa
kwa watanzania.
Mwishoo,
Comments