CHAMA cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga kimepata viongozi wapya wataongoza
chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano katika uchaguzi uliofanyika
jana.
Katika
nafasi ya Mwenyekiti Wilaya imechukuliwa na Ally Msikamo kwa kura 749
baada ya kuwashinda wagombea wawili , Abdallah Kihato kura 189 na
Mbaraka Mahanaka kura 44.
Nafasi
ya katibu Mwenezi Wilaya imechuliwa na Ben Mkulia kwa kura 89 na
kuwabwaga wagombea wawili , Mchowi aliyepata kula 22 na Ali Ngalema kula
Saba (7).
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya Mkuranga , Ali Msikamo amesema
kuwa uchaguzi umeisha na kilechobaki ni kufanya kazi katika ya kuendesha
chama katika kumsaidia Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Amesema
kazi ya chama kazi ya chama wilaya kuishauri serikali katika kusaidia
chama kuendelea kushika dola ikiwemo na maandalizi ya uchaguzi mkuu.
Mbunge
wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa uteuzi wa Naibu Waziri
umetokana na wananchi wa Mkuranga na sio ujanja wake mwenyewe ndio
uliomfanya aonekane.
Amesema
kuwa maendeleo ya Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi
kuandaliwa mkutano utaohusisha wajumbe wote kuangalia walikotoka na
wanako elekea.
Mwenyekiti
mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo
akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Wilaya kwa kumpa
ridhaa ya kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka miatano.
Mbunge
wa Mkuranga , Abdallah Ulega alieapishwa leo kuwa Naibu Waziri wa Uvuvi
na Mifugo, akizungumza katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa Wilaya ya
Mkuranga.
Sehemu ya viongozi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi.
Picha mbalimbali za uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Comments