UONGOZI wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen umeungana na ndugu wa majeruhi 9 na wafiwa wa vifo vya watu 15 vilivyotokea katika ajali ya lori aina ya fuso eneo la Ntembwa, Wilayani Nkasi.
Katika kuhakikihsa tukio hilo halijirudii Mh. Zelote amepiga marufuku ukiukwaji wa sheria ya kupandisha abiria katika magari ya mizigo na kuonya kuwa yeyote atajayefanya hivyo achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.
“Nimekataza binadamu kugeuzwa kuwa ni mifuko ya misumari, ni bora tubakie na wananchi wetu salama, watu wasipande kwenye malori, nimefikiria ni vyema tutumie zile chai maharage kuliko kupanda kwenye malori,” Alisisitiza.
Mh. Zelote alifika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupokea habari hiyo ili kuweza kusaidia na kuhakikisha maiti na majeruhi hao wanapatiwa huduma stahiki na kufanikisha zoezi la uokoaji.
Ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 425 BFF kuacha njia na kupinduka ilitokana na mwendo kasi wa dereva uliochangiwa na ugeni wa barabara hiyo.
Lori hiyo mali ya Bakari Ali Kessy iliyokuwa imetokea Kijiji cha Mvimwa kuelekea Kijiji cha Wampembe ilikuwa imepakiwa shehena ya viroba vya mahindi na watu iliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo vya watu 15 kati yao wanawake 10 na wanaume 05.
Waliofariki katika ajali hiyo ni
1. Domona Tenganamba, 41yrs, mfipa mkulima.
2. Emmanuel Rashid 84yrs, mfipa mkulima, mkazi wa ntemba
3. Restuta Sunga , 35yrs, mfipa mkazi wa ntemba
4. Salula Revana 64yrs, mfipa mkazi wa mtapenda isale
5. Ferisia Tenganamba , miaka 1 – 6/12
6. Prisca Madeni, 45yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa china
7. Richard Chikwangara, 24yrs, mfipa, mwalimu mkazi wa kalambanzite
8. Yusta Somambuto, 36yrs, mfipa, mkulima mkazi wa kizumbi
9. Gilesi Ramadhan, 24yrs, mfipa, mkulima mkazi wa sumbawanga
10. Odetha Madirisha 46yrs, mfipa mkulima wa kizumbi
11. Megi Nalunguli, 52yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
12. Abuu Amani @ mandevu, 37yrs, muha, biashara, mkazi wa liapinda
13. Nyandindi Batrahamu, 35yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa sumbawanga
14. Magdalena Mbalamwezi, 50yrs, mfipa, mkulima mkazi wa ntuchi
15. Mtoto mchanga wa wiki mbili, mwanaume ambaye hajapewa jina
Majeruhi wa ajali hiyo ni:-
1. Dismas Clement, 26yrs, mfipa, mkulima mkazi wa mwinza
2. Sema Savery 25yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
3. Ally Haruna, 33yrs, mfipa, mkazi wa namanyere
4. Yusta Mfundimwa, 50yrs, mkulima mkazi wa izinga
5. Tenesfory Oscar, 36yrs, mfipa mkazi wa wampembe
6. Amos Kitambale, 25yrs, mfipa, mkazi wa wampembe
7. Neema Mwanandenje, 21yrs, mfipa, mkazi wa mlambo
8. Joseph Sungula, 28yrs, mfipa, mkulima.
9. Majeruhi mmoja mwanamke ambaye hajafahamika kwa jina yuko icu
Baada ya kusababisha ajali hiyo dereva alitoroka lakini juduhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea kufanyika.
Abate wa Pambu Martin Mkolwe Abasia ya Mvimwa akiongoza ibada fupi ya kuwaombea marehemu wa ajali iliyoua watu 15 na kujeruhi 9 iliyofanyika katika kituo cha afya Mvimwa, Wilayani Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kaunda Suti ya ugoro) akitoa salamu zake za pole kwa wafiwa, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda na kulia kwake ni Abate Pambu Mkolwe wa Abasia ya Mvimwa.
Comments