Skip to main content

HAWA HAPA WANAHARAKATI WA GDSS



Wanaharakati mbalimbali wa jiji la Dar es salaam ambao pia ni washiriki wa semina za jinsia na maendeleo(GDSS) wamekutana mapema wiki hii kujadili sera ya ardhi ya mwaka 2016.
Muwezeshaji wa semina ya GDSS wiki hii Bw. Kumbuka Mwakyusa kutoka shirika la Haki Ardhi akitoa elimu kwa wanaharakati kutoka kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam
Semina hiyo iliyoongozwa na wawezeshaji wawili kutoka taasisi ya watu binafsi ya Haki Ardhi akiwemo Kumbuka Mwakyusa na Vickness Dickson wakiwapa elimu wanaharakati hao tangu kuanza kwa mchakato huo mpaka kukamilika na mapungufu yanayopatikana katika sera hiyo.

Kwa mujibu wa wawezeshaji inaonyesha kuwa mfumo wa upatikanaji wa sera hiyo sio rafiki kwa wananchi wa hali ya chini kwani katika mchakato wa kutengeneza sera hiyo haukuwahusisha na badala yake wamechukua viongozi wakubwa wasiojua matatizo ya wananchi hao.
Bw. Kumbuka Mwakyusa akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika semina iliyofanyika mapema wiki hii makao makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Lakini pia mchakato huo haukukidhi matarajio ya wananchi wadogo kama wakulima, wafugaji, wavuvi nk. Kwani haukuwa shirikishi kama mchakato wa mwaka 1995 ambao ulijikita katika kuingia kijiji kimoja baada ya kingine kuchukua maoni ya wananchi.

Aidha wawezeshaji hao walisema kuwa mchakato huo ulifanyika kimya na kwa siri kiasi kwamba wananchi wengi hawakuwa na taarifa hivyo idadi ndogo sana ilipata nafasi ya kushiriki, lakini pia hao waliopata nafasi ya kushiriki maoni yao hayakuchukuliwa yote.
Mwanaharakati wa GDSS Bi. Subira Kibiga akichangia mada katika semina iliyofanyika mapema wiki hii makao makuu ya Mtandao wa Jinsia (TGNP).
Lakini pia imeelezwa kuwa sera hii haikuwa na lengo zuri la kuwakomboa wananchi wadogo kwani imeeleza kuwa mwananchi anapohitaji mkopo anatakiwa kuweka rehani ardhi yake, na hii inahesabiwa ni kama njia ya kutaka kuwapokonya ardhi wananchi hawa pale wanaposhindwa kulipa deni.

Na jambo lingine ni kwa wananchi wa vijijini kulazimishwa kulipa kodi wakati toka zamani utaratibu huu haukuwepo kwa kuwa inafahamika wananchi wa vijijini hali zao ni duni, na wakigoma wanaambiwa hawajui umuhimu wa ardhi yao na kutishiwa kupokonywa.
Bi. Vickness Dickson muwezeshaji wa pili kutoka shirika lisilo la kiserikali la Haki Ardhi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika semina ya wanaharakati wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS) mapema wiki hii.
Na pia sera hiyo imeipa mamlaka makubwa serikali ya kumiliki ardhi za vijiji na sio kama hapo mwanzo wananchi walimiliki ardhi yao kwa kupitia serikali zao za vijiji, na kudai kwamba viongozi wa vijiji hawana utaalamu wa kutosha hivyo kupewa kamishna kutoka serikalini aongoze zoezi hilo, lakini pia hii imeonekana kuwa itachochea mianya ya rushwa.

Kutokana na changamoto hizo zote wawezeshaji na wanaharakati walipitisha mapendekezo yafuatayo na kwanza ni kuondolewa mapango wa kodi kwa wananchi hao lakini pia kupewa elimu kupitia viongozi wao wa vijiji juu ya umiliki ardhi yao na mali asili.
Ndugu Abadallah Matata akitoa mchango wake katika semina ilikuwa ikijadili kuhusu mchakato wa sheria ya ardhi ya mwaka 2016.
Lakini pia mikutano ya vijiji iwe na maamuzi juu ya ardhi yao na kupewa elimu juu usimamizi wa ardhi yao na kupunguziwa nguvu aliyopewa muwekezaji lakini pia kutopewa hati ya umiliki kwani atanyanyasa wananchi wa kijiji husika.

Sharia hii haijatoa ukomo kwa muwekezaji kuwa anatakiwa kumiliki kiasi gani cha ardhi hivyo wao wamependekeza asipewe zaidi ya ekari 200 kwa ardhi ya vijiji na  kama atahitaji kwa vijiji tofauti basi zigawanywe ekali hizo lakini isizidi kiwango hicho na ikishindikana aombe kwenye ardhi ya jumla siyo ya kijiji tena.

Baadhi ya washiriki wa semina ya GDSS wakifuatilia kwa umakini semina hiyo

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...