Mkuu wa mkoa waDar es Salaam, Paul Makonda(katikati) pamoja na mkuu wa wilaya ya kinondoni(kushoto)
Mh.Makonda pamoja na mkuu wa wilaya ya ilala Sophia Mjema(kushoto) wakati wakifanya ziara Maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Picha zikionyesha hali na jinsi Mvua ilivyosababisha maafa Maeneo aliyofanya Ziara hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amefanya Ziara ya kukagua miundombinu iliyoathiriwa na Mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha na kusema Serikali itakarabati mara moja miundombinu yote iliyoathiriwa na Mvua.
Katika ziara hiyo MAKONDA ameambatana na Kamati ya Maafa ya Mkoa ambapo wametembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na Mvua ikiwemo Jangwani, Daraja la Malecela,Daraja la Korongo, Daraja la Tandale kwa Mtogore, Africana na Boko Basihaya na kutoa pole kwa Wahanga.
Aidha Makonda amewataka Wananchi waliojenga kwenye maeneo hatarishi kuchukuwa tahadhari mapema kwakuwa Wataalamu wa hali ya Hewa wametangaza kuwa Mvua kubwa zitaendelea kunyesha. Kwanzia November Mosi mwaka huu.
Amesema kuwa Ujenzi wa Miundombinu iliyoharibiwa ikiwemo ya Maji,Umeme,Mitaro, Barabara na Madaraja inaendelea kurekebishwa ambapo katika Daraja la Malecela ameagiza kujengwa Daraja la Muda mfupi na Vijana kutoka Jeshi la Wananchi.
Amesema zaidi ya Shilingi Billion Moja zimetolewa na Bank ya Dunia kwaajili ya Maboresho ya eneo la Jangwani ambapo Serikali ya Mkoa ina vifaa vya kutosha kwaajili kuokoa Wananchi.
Amesema katika mto Ng'ombe uliopo Tandale kwa mtogole utajegwa na wanaopaswa kulipwa fidia watalipwa kulingana na Maeneo yao.
Pia ameongeza kuwa miongoni mwa Sababu zilizopelekea Maji ya mvua kukosa mwelekeo ni Ujenzi holela, Uchimbaji wa Mchanga na watu kutupa taka hovyo kwenye Mito.
Miongoni mwa Wilaya alizotembelea ni pamoja na Ilala, Ubungo na Kinondoni ambapo kuna Nyumba zaidi ya 200 zipo kwenye mazingira hatarishi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari mapema kwani kinga ni bora kuliko tiba.Chanzo kimoja kimeripoti.
Comments