MSANII wafilamu na tasnia ya tamthiliya nchini Rakheem David amepanga
kuwapa raha mashabiki wake katika uzinduzi wa
ujio mpya wa filamu iitwayo 'Mammu'.
Katika usiku wa uzinduzi huo Rakheem ameuambia mtandao huu Dar es Salaam
jana kuwa uzindzi huo utafanyika King D Hotel iliyopo Sinza maeneo ya Afrikasana.
"Katika uzinduzi wangu nimejipanga kwa watakao fika watapita kwenye
Red Carpet sambamba na kufanya mahojiano, "alisema Rakheem.
Rakheem alisema mara baada ya kua nimekamilisha uchukuaji wa picha
katika filamu yangu kuwa kamili kuingia sokoni, kampuni ya Afrocinema
Tours Campany chini ya Richard Kabisi ndio iliyoongea nami kuhusu kufanya
uzinduzi na nitaanza kuisambaza filamu yangu mwenyewe mara baada ya uzinduzi.
Aidha Nyota huyo ambaye tayari ni mwenye umaarufu,awali amewahi kufanya
vema katika filamu kama iliyoitwa 'kibajaj iliyoshirikisha nyota wengine
kama Motorola, Irene Poul pamoja na nyingine iliyoitwa 'Mama Ntilie '
iliyoshirikisha nyota kama Gabon, King Majuto pamoja na Irene Poul.
Rakheem ameweza kufanya kweli pia kupitia tamthiliya ya Duty inayooneshwa
kupitia Star Tv kila siku za jumatano saa 1:00 usiku.
Comments