SHIRIKA la Posta limesema litatoa msaada wa matibabu kwa watoto wawawili wanaohitaji msaada wa matibabu katika hospitali ya Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam.
Pichani ni Mkuu wa Posta
nchini Deogratius Kwiyukwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
juzi kuelekea maadhimisho ya Posta Duniani.
Hiyo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Posta nchini Deogratius Kwiyukwa juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mahazimisho ya kushehelekea siku ya kuzaliwa Umoja wa Mashirika ya Posta Duniani Oktoba 9 mwaka huu.
Alisema siku hiyo ilianza kuadhishwa kwa mara ya kwanza katika mkutano Mkuu wa wanachama wa umoja huo mwaka 1969 baa da ya makubaliano yaliyofanyika mwaka huo mjini Tokyo Japan.
"Kupitia Mkurugenzi huyo wa Umoja wa Posta Duniani, kila mwaka hutoa ujumbe maalum kwa nchi zote wanachama ambao nia yake ni kuchochea maendeleo kwa kuonesha mwelekeo wa huduma za Posta kwa dunia ya sasa,"alisema Deogratius.
Deogratius alisema maadhimisho ya Posta Duniani huambatana na shughuli mbali mbali za kijamii kama vile kutoa misaada kwa jamii na kwa wasio jiweza.
Aidha alisema Kuwa Shirika la Posta Tanzania mwaka huu mbali na kusoshiriki katika kuelimisha Umma juu ya shughuli mbali mbali kupitia vyombo vya habari wameweza kuwaalika wanafunzi kutoka shale za msingi ili kuwaelimisha juu ya juu ya shughuli za Posta.
Pia Mkurugenzi huyo alisema shirika litaendelea kuunganisha mfumo wa mawasiliano ambao ni on-line katika ofisi zote za Posta nchini ili kutoa huduma kwa ufanisi zaidi ,kuongeza idadi ya wateja na kuondoa uchelewesho na kupunguza malala miko.
Alisema kwa hivi sasa vimeisha unganishwa vituo 114 na vingine 15 vitaunganishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Deogratius alisema shirika limeweka msukumo na ushawishi maalum katika uanzishwaji wa vituo hivyo ilikuwezesha huduma za utawala serikalini kufanyika katika sehemu moja ikiwa ni pamoja na ulipaji ulipaji wa kodi na ada mbali mbali na kwa ujumla Kuwashirikisha wananchi katika uendeshwaji wa shughuli za serikali yao.
Shirika la Posta nchini limejipambanua katika muktadha huo likiwa limelenga kusimamia miundo mbinu mipya ya kiteknlojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) hususan malipo mtambuka ambapo miundo mbinu hiyo itaboresha huduma zinazotolewa sasa na nyingine za kiselikari.
Comments