Pichani ni Mkurugenzi wa halimashauri ya Mbulu Hudson Kamoga akiwa Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Conversation Centre ulipo
fanyika mkutano huo wa (ALAT )Dar es Salaam.
MKurugenzi wa halimashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara Hudson Kamoga amesema kuwa agenda za mkutano wa 33 wa Jumuiya ya tawala za Mitaa nchini (ALAT) uliofanyika hivikaribuni Dar es Salaam na kufunguliwa na mgeni rasmi mwenye dhamana ya serikali Rais John Pombe Magufuli ulikua na tija.Hayo yamesemwa na Kamoga jijini Dar es Salaam sikuchache zilizopita ambapo alisema kaulimbiu ya mkutano ilizingatia kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuhusu sekta ya viwanda.
Alisema wakati wa mkutano huo waliweza kukutana na viongozi mbali mbali nakujadiliana na kukamilishana mawazo kwani miongoni mwa walikuwa wakitoka maeneo ya mjini na vijijini na kuzungumzia changa moto mbali mbali.
"Anampongeza Rais Magufuli kauli zake alizozitoa katika ufunguzi wa mkutano huo kwani zina lengo la kuijenga taifa katika kufikia uchumi wa viwanda ,"alisema Kamoga.
Alisema mkutano huo wa 33 ulikuwa kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa mamlaka za serikali za mitaa (ALAT ).
Ajenda za mkutano huo zilikua ni pamoja na kupisha mipango na bajeti ya Jumuiya kwa mwaka wa fedha 2017 na 18 na kujadiliana hasa fursa na changa moto katika uendeshwaji wa mamlaka za mita.
Comments