Famous Furniture,Wasambazaji wa Magodoro ya Sealy Posturepedic na Masofa ya La-Z-Boy Wafungua Duka Dar es salaam
FAMOUS Funiture waelezea malengo makubwa waliyonayo katika kukua kwa uchumi wa viwanda ambapo wamewataka watanzania kutumia bidhaa bora za la-Z-Boy ambazo zimeboreshwa zaidi kwa muonekanao wa nyumbani.
Hayo yalisemwa na Meneja wa duka hilo Nabeel Dharser ambaye ni meneja wa duka la thamani za nyumbani wakati wa uzinduzi wa duka hilo oktoba 18 mwaka huu wakati wa udhinduzi Mliman City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Sofa za la-Z-Boy kutoka Famous Furniture.
Nabeel alisema kuwa Famous Furniture Limited iliyosajiliwa na namba 135127 iliona umetambulisha bidhaa bora za nyumbani Ili kukidhi soko linalokuwa nchini hapa.
"Binadamuhutumia muda mwingi wakiwa wamekaa chini,hii ndio sababu ya wabunifu,watafiti na wataalamu wa afya kuumiza vichwa kutoa bidhaa zitakazoleta starehe,"alisema Nabeel.
Baadhi ya viti vya La-Z-Boy kutoka Famous Furniture.
Mmoja wa wateja walioudhuria ufunguzi akijaribu kulala kwenye godoro la Sealy Posturepedic
Nabeel alisema mbali na uzinduzi wa huo, duka hilo wanatarajia kufungu maduka mengine 5 maeneo mengine Tanzania.
Aidha kwa upande wake meneja wa Bravo Group Bw.Ryan Beattile ambao ni wasambazaji wa La-Z-Boy kutoka Famous Furniture aliongeza kuwa starehe ya mkao sio katika muonekano tu bali ni kuupa starehe mwili sambamba na mfumo bora egemezi, hasa kama unakaa kwa muda mrefu.
Comments