Shahidi wa kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili Muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Binadamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dtk. Innosent Mosha ambaye ni shahidi wa nne wa kesi hiyo amesema kwamba baada ya kumpima ubongo marehemu Kanumba waligundua kuwa umevimba.
Akitoa ushahidi huo leo mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeelezwa kuwa Daktari huyo aliletewa oda kutoka Jeshi la Polisi kwamba aufanyie uchunguzi mwili wa Steven Kanumba uliokuwa mochwari akishirikiana na daktari mwingine.
Dkt. Mosha amesema kwamba “Tulifungua ubongo wa Kanumba na kuukuta umevimba, mishipa midogomidogo ya ubongo ilikuwa imeingia damu, lakini kabla ya kufungua ubongo, kwenye kisogo kulikuwa na mgando wa damu" Dkt. Mosha.
Ameongeza kwamba “Baada ya kumaliza uchunguzi wetu tulipeleka sampuli kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo tulipeleka pia sampuli mbalimbali za viungo vya mwili wake,” amefafanua Dkt. Mosha.
Baada ya Mashahidi kutoa ushahidi wao Mahakama imesema kuwa Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma za kifo cha msanii Steven Kanumba , hivyo anatakiwa kujitetea
Comments