KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) imesema kwa kushirikiana na Wizara ya mambo ya Nje
na ushirikiano wa Afrika Mashariki,Taasisi sekta binafsi Tanzania (TPSF) na
Ubalozi wa Tanzania nchini China iimeandaa kongamano maalum la kuhamasisha
na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na China katika kongamano
hilo linatarajiwa kufanyika Oktoba 16 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Geofrey
Mwambe alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana ambapo alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kutangaza fursa za biashara na uwekezaji
zilizopo hapa nchini kwa wawekezaji na wafanya biashara wa China fursa ambazo zipo
katika sekta mbali mbali kama vile viwanda ,Madini ,Nishati,Usafiri,Mafuta na pamoja
na Miundombinu.
Alisema sekta zingine ni ujenzi ,uvuvi wa kina kirefu,Kilimo na usindikaji wa
mazao,Afya,Teknolojia ya habari na mawasiliano,Madawa. mbali na hayo.
TIC pia kimekanusha taarifa zilizoenea kuwa wawekezaji
wanafunga biashara zao huku kikibainisha kuwa taarifa hizo ni za uongo na
zinafaa kupuuzwa kwani wawekezaji wanaendelea kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza
kwenye sekta mbalimabli.
"China mpaka Mei mwaka huu inaongoza kwa uwekezaji nchini kwa thamani ya
miradi na tunatarajiwa kongamano hili kuhudhuriwa na wawekezaji wa makampuni
makubwa zaidi ya 100 kutoka China,"alisema Geoffrey.
Geoffrey alisema China itasaidia kuiweka na kuitangaza Tanzania kama miongoni
mwa maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kibiashara kwa kampuni za kutoka
China.
Aidha alisema makampuni ya kitanzania yanakaribishwa kushiriki kwenye kongamano
hilo ili kuweza kuanzisha , kukuza na kuendeleza ushirikiano katika nyanja za biashara
na uwekezaji kwa kushirikiana na kampni za wafanya biashara wa China.
"Tunategemea Tanzania ita ongeza thamani ya mitaji ya uwekezaji kutoka nje yaani
FDI iwapo makampuni ya China yatakayohudhuria kongamano yata amua kufanya uwekezaji
nchini,"alisema Geoffrey.
Alisema TIC inapenda kutumia fursa hiyo kuitangaza Tanzania kwa ujumla kwani
mpaka sasa mwezi Mei mwaka huu kituo cha uwekezaji TIC,kimeweza kusajili miradi
670 ambayo yenye umiliki wa china inayotarajia kuzalisha ajra zipatazo 83,394 yenye
thamani ya mtaji wa kiasi cha dola za Marekani 5,779 hivyo hiyo ni fursa muhimu kabisa
kwa watanzania.
Comments