Mkuu wa mkoa waDar es Salaam, Paul Makonda(katikati) pamoja na mkuu wa wilaya ya kinondoni(kushoto) Mh.Makonda pamoja na mkuu wa wilaya ya ilala Sophia Mjema(kushoto) wakati wakifanya ziara Maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam. Picha zikionyesha hali na jinsi Mvua ilivyosababisha maafa Maeneo aliyofanya Ziara hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amefanya Ziara ya kukagua miundombinu iliyoathiriwa na Mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha na kusema Serikali itakarabati mara moja miundombinu yote iliyoathiriwa na Mvua. Katika ziara hiyo MAKONDA ameambatana na Kamati ya Maafa ya Mkoa ambapo wametembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na Mvua ikiwemo Jangwani, Daraja la Malecela,Daraja la Korongo, Daraja la Tandale kwa Mtogore, Africana na Boko Basihaya na kutoa pole kwa Wahanga. Aidha Makonda amewataka Wananchi waliojenga kwenye maeneo hatarishi kuchukuwa tahadhari ma...