Skip to main content

Posts

Hamis Mnyupe amerejea kwenye bendi yake ya zamani

MPULIZAJI tarumbeta nguli, Hamis Mnyupe amerejea kwenye bendi yake ya zamani ya Msondo Ngoma Music Band na tayari ameanza kuonekana kwenye shoo za bendi hiyo tangu wiki iliyopita. Mnyupe aliyewahi kuitumikia Msondo Ngoma kwa zaidi ya miaka kumi na tano, aliipa kisogo bendi hiyo takriban miaka miwili iliyopita, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni maslahi na kubadilisha upepo. Kiongozi mwandamizi wa Msondo Ngoma, Juma Katundu ameiambia Saluti5 baada ya kuona kwamba bendi yao inazidi kuandamwa na pengo kubwa la wapulizaji wa ala za upepo. “Hivi sasa ndani ya Msondo Ngoma kwenye ala ni kama tumebaki na Romario peke yake baada ya mwenzake, Ibrahim Mwinchande kufanyiwa upasuaji wa ngiri unaomlazimu kupumzika kazi kwa muda,” amesema Katundu.

Nigeria yaongeza nguvu kuwasaka wasichana waliotekwa

Image caption Wasichana wa Chibok walitekwa pia mwaka 2016 kwa mtindo kama wa sasa Mamlaka nchini Nigeria imesema imeongeza nguvu ya ndege za kivita ili kuweza kuwasaka wanafunzi wasichana waliotekwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Serikali inasema takriban wasichana 110 hawajulikani walipo baada ya wanamgambo wa kiislam kuwateka katika shule yao iliyopo Dapchi. Mapema serikali ya kijiji hicho ilililaumu jeshi kwa kushindwa kuchukua hatua hata baada ya kupewa taarifa. Rais Muhammadu Buhari ameelezea tukio hilo kama janga la taifa. Vikosi vya Nigeria vyashindwa kumkamata Shekau Serikali ya Nigeria yaomba radhi utekwaji wasichana Hasira zimekuwa zikiwapanda wazazi wa wasichana hao huku kukiwa na ripoti kuwa wanajeshi walikuwa wameondolewa kutoka kwa vizuizi vikuu vya Dapchi mwezi uliopita. Dampchi ambao ni mji ulio kilomita 275 kaskazini magharibi wa Chibok, ulishambuliwa siku ya Jumatatu, na kusababisha wanafunzi na walimu kutoka shule moja ya serikali kukimbili...

Mbunge wa Mbeya Mjini amehukumiwa kufungwa jela miezi mitano

Haki miliki ya picha Image caption Bw Joseph Mbilinyi (wa kwanza kushoto) Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema Joseph Mbilinyi kwa jina maarufu Sugu na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya nyanda za juu kusini, Emmanuel Masonga wamehukumiwa kufungwa jela miezi mitano. Wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli. Mbunge aliyedaiwa kumtusi Magufuli apewa dhamana Tanzania Je ni ''utumiaji mbaya wa mamlaka'' Tanzania? Wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi Desemba mwaka mwaka jana jijini Mbeya. Hukumu dhidi yao imetolewa na Mahakama ya hakimu mkazi jijini Mbeya. Hati ya mashtaka imesema maneno waliyoyatamka yalienda kinyume na Sehemu 89(1) a ya Sheria za Jinai ambayo inaharamisha kutumiwa kwa lugha ya matusi. Maneno hayo, hati za mashtaka zinasema, yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Salah amefunga magoli 30 katika mechi 36

Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amempa 'tano' kocha wake Jurgen Klop kwa mafanikio anayoyazoa msimu huu. Salah amefunga magoli 30 katika mechi 36 za michuano yote katika msimu wake wa kwanza na Liverpool na ni mchezaji anayeshika nafasi ya pili kwa upachikaji mabao Premier League akiwa na magoli 22, nyuma ya Harry Kane mwenye magoli 23. "Liverpool nimekuwa nikicheza jirani zaidi na lango la adui, kocha wangu amenitaka nicheze hivyo, hatua inayoniwezesha kupachika magoli mengi," anaeleza Salah na kuongeza:  "Sikuwahi kupewa fursa hiyo katika klabu nyingine yoyote ile au kwa kocha mwingine kabla ya kukutana na  Jurgen Klop"

Isaac Drogba mwendo mdomdogo alijiunga na Guingamp akiwa ana umri wa miaka 16 tu

Isaac Drogba (kushoto), mwenye umri wa miaka 17, mtoto wa gwiji wa soka, Didier Drogba akikabidhiwa jezi ya klabu yake mpya,  Guingamp ya Ligue 1 jana  moja ya timu alizochezea baba yake mwanzoni mwa maisha yake ya soka nchini Ufaransa.  Drogba mkubwa alijiunga na Guingamp akiwa ana umri wa miaka 16 tu kwa ada ya uhamisho ya Pauni 80,000 kutoka Le Mans.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera akaribishwa kupata kupata uzoefu katika Mtaa wa Kongo Kariakoo jijini Dar es Salaam

 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera akisalimia wananchi baada ya kutambulishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (watatu kushoto) alipowapeleka Kasesera na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma Abdallah katika eneo la biashara za Machinga katika Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kupata uzoefu wa namna Wilaya ya Ilala ilivyofanikiwa katika kuboresha mazingira na kuwaweka pamoja machinga hao katika shughuli zao. Wapili kushoto ni Katibu Tawala wa Ilala Edward Mpogolo.  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma Abdallah kwa Machinga wakati wa ziara hiyo  Baadhi ya kinamama wakimweleza kero Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alipokuwa na ugeni huo  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera akiwa katika Mtaa wa Kongo kujionea shughuli mbalimbali zinavyoendesha na Machinga wa Kariakoo  Msafara wa  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera ukipita katika mitaa ...