KATIKA Live
Chumba cha Habari Global Publishers, leo tunaye mwanamuziki mahiri
anayefanya vizuri ndani na nje ya Tanzania, Ambwene Yessaya ‘AY’ au Mzee
wa Commerial ambaye amesema sasa hivi amekuwa wakala wa wasanii wa
ndani na nje ya nchi.GPL
Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Ambwene Yessaya 'AY' akipozi katika studio za Global TV Online kabla ya kuhojiwa.
Katika
mahojiano na safu hii ambayo huwa inarushwa kupitia Global Tv Online
kwenye Kipindi cha Mtu Kati, AY aliweka wazi kuwa anafanya muziki kwa
ajili ya watu wote.Mwandishi: Unakumbuka nini kupitia kundi lako la
zamani la East Coast Team ambayo sasa hivi haipo tena?
AY: East
Coast Team bado ipo, kitu ambacho nakumbuka sisi tulikuwa marafiki na
muziki ulitufanya tukawa kama ndugu, nilitoka mwaka 2006 kwa ajili ya
tofauti za kimisimamo na kimtazamo, baadaye MwanaFA naye akaja kutoka.
Baada ya
kuachana bado tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana lakini kila mtu
anafanya kazi katika njia yake na mpaka sasa hivi wenyewe bado
wanaendelea kama East Coast Team pia kuna ‘project’ ambayo tutakuja
kuifanya pamoja mwakani.
Mwandishi: Inasemekana uko zaidi na MwanaFA kuliko GK kuna nini hapo kati?
AY: Wakati natoka nilibakia kuwa AY na MwanaFA kama MwanaFA na mimi na MwanaFA ni washikaji kama ‘brothers’, ndiyo maana tumeshirikiana kwenye project nyingi zaidi baada ya kutoka nje. Sisi siyo kundi lakini kila mtu ni mwanamuziki wa kujitegemea.
AY: Wakati natoka nilibakia kuwa AY na MwanaFA kama MwanaFA na mimi na MwanaFA ni washikaji kama ‘brothers’, ndiyo maana tumeshirikiana kwenye project nyingi zaidi baada ya kutoka nje. Sisi siyo kundi lakini kila mtu ni mwanamuziki wa kujitegemea.
Mwandishi:
Mbali na muziki wewe ni meneja ambaye unamiliki wanamuziki wengi ndani
na nje ya Tanzania, kwa sasa una wasanii wangapi?
AY: Sasa
hivi nimekuwa wakala, kampuni yangu inafanya kazi ya uwakala na wasanii
wengi nje na ndani. Miongoni mwao ambao nimeshawahi kufanya nao kuna
Nameless, Stereo, Ommy Dimpoz, Chameleone, P-square na wengine wengi.
Kampuni kama hizo zipo katika kila nchi kwa hiyo na mimi nikaona bora
nifungue.
Mwandishi: Changamoto gani unakumbana nazo katika biashara zako?
AY:
Biashara yoyote ina changamoto na inakufanya akili yako inakuwa
inapanuka zaidi na unaweza kujifunza mbinu nyingi kupitia changamoto
uliyoipata. Kiukweli tunajitahidi mimi pamoja na wenzangu tunaona jinsi
matunda ya kazi yetu tunayoifanya.
AY akiwa ndani ya studio za Global TV Online na prizenta Pamela Daffa 'Pam D'.
Mwandishi: Unahisi ni sababu gani zinawafanya vijana wengi kushindwa kutoboa kimataifa?
AY: Hii
kitu nilikuwa naiangalia tangu zamani ndiyo maana naona nikiendelea
kushikilia vitu vya zamani nilivyokuwa navifanya nisingeweza kufikisha
vitu ambavyo vinafanyika leo.
Nilivyoingia
kwenye muziki nilikuwa nataka siku ambayo naacha muziki watu
wanikumbuke kwa kitu fulani, lazima muziki ubadilishe maisha yangu ndiyo
maana unaona najitahidi kuwavuta wasanii wenzangu kuwapa chaneli na
netiweki zingine kwa ajili ya kwenda mbali zaidi.
Mwandishi: Nini siri ya mafanikio yako?
AY: Vyote hivi ni kuipenda kazi uwe na heshima nayo yaani ujiheshimu na pia uwe na mtandao ujue jinsi ya kufahamiana na watu.
Mwandishi: Ulijisikiaje kufanya kazi na Sean Kingstone?
AY: Nilijisikia vizuri sana kwani mefanya kazi na msanii ambaye zamani nilikuwa namuona kwenye runinga sikuwa na mawazo ya kuja kukutana naye na kufanya naye kazi, kizuri zaidi yeye ndiyo alipendekeza nifanye naye kazi nakumbuka alikuwa amekuja hapa na akaona kazi zangu na alivyokwenda kufanya mahojiano kwenye redio nilikuwa nasikiliza siku hiyo nikashangaa ananitaja mimi bila kujua.
AY: Nilijisikia vizuri sana kwani mefanya kazi na msanii ambaye zamani nilikuwa namuona kwenye runinga sikuwa na mawazo ya kuja kukutana naye na kufanya naye kazi, kizuri zaidi yeye ndiyo alipendekeza nifanye naye kazi nakumbuka alikuwa amekuja hapa na akaona kazi zangu na alivyokwenda kufanya mahojiano kwenye redio nilikuwa nasikiliza siku hiyo nikashangaa ananitaja mimi bila kujua.
Mwandishi: Ni hatua gani ambayo unaikumbuka imekupa mafanikio?
AY:
Nakumbuka Profesa J wakati anazindua albamu yake ya Machozi, Jasho na
Damu, akanipa kolabo katika albamu yake wakati nikiwa na ngoma ya Raha
Tu, akaniambia wimbo unaitwa Nawakilisha nataka ‘verse’ kesho yake
nikawa tayari basi tukaanza kuzunguka na ndiyo ‘tour’ iliyonifanya
nikaanza kufahamika Tanzania nzima, kufahamiana na watu zaidi na mpaka
leo tunashirikiana vizuri.
Mwandishi: Sasa hivi umesimama kutoa albamu, unakumbuka una albamu ngapi mpaka sasa?
AY:
Nimeacha kutoa albamu tangu mwaka 2006 miaka 8 iliyopita, ya kwanza
ilikuwa inaitwa Raha Kamili 2003, Hisia Zangu 2005, Habari Ndiyo Hiyo
niliyoifanya na MwanaFA. Nafanya muziki kwa ajili ya watu wote, nafanya
kama AY lakini bidii zangu pia hata wasanii wengine wanafaidika nazo,
tusapotiane tuweze kusonga mbele, tuwe na upendo kati yetu,
tusipandikiziane chuki kati ya wasani kwa wasanii ili twende pamoja,
tufike mbali zaidi.
Comments