Mkuu wa
wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selengu akimkabidhi kadi ya kujiunga na
Mfuko wa Afya ya Jamii CHF mmoja kati ya wakulima wa tumbaku katika
kijiji cha Kisanga wilayani humo wakati wa kampeni ya Uzinduzi wa mfuko
huo.
Mkuu wa wilaya ya Sikonge akikabidhi kadi ya CHF kwa mkazi wa kijiji cha Kisanga wilayani humo
Baadhi ya
wananchi wa kijiji cha Kisanga waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo
ya uhamasishaji kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wilayani Sikonge.
Wananchi
wakiwa wamekaa chini ya mti wa Mwembe wakisiliza kwa makini maelezo
kuhusu faida za kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF,wakati wa
uhamasishaji mfuko huo.
Meneja wa
mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kanda ya Magharibi Bw.Emmanuel
Adina akigawa vipeperushi kwa wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Mfuko
wa Afya ya Jamii CHF katika kijiji cha Kisanga.
Meneja wa
Mfuko wa Taifa wa Bima Afya NHIF kanda ya Magharibi Bw.Emmanuel Adina
akitoa ufafanuzi kuhusu kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii.
Na Juma Kapipi-Sikonge,KAPIPIJhabari.COM
JAMII imeshauri kubadilika na kujenga
tabia ya kuchangia matibabu kupitia mifuko ya (NIHF) na (CHF) na
kuachana na tabia ya kupenda kuchangia sherehe pekee badala yake wajitoe
kuchangia na matibabu.
Meneja
wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NIHF) kanda ya magharibi Emmanuel
Adina alisema hayo wakati akiongea na wananchi wa kata ya Kisanga wilaya
ya Sikonge mkoani Tabora siku ya uzinduzi wa mfuko wa afya ya jamii
(CHF).
Adina
alisema jamii imejenga tabia ya kupenda kuchangia harusi na sherehe
nyinginezo tena kwa kiwango kikubwa lakini linapokuja suala la kuchangia
mifuko ya afya kwa ajili ya kupata matibabu bora jambo hilo linakuwa
zito.
Alisema
kiwango cha uchangiaji kwa wilaya ya Sikonge ni sh 5,000 na matibabu
yatapatikana kwa muda wa miezi 12 kwa mume,mke na watoto nane.
Adina
alisema afya ni jambo muhimu duniani na kama taifa lolote halina jamii
yenye afya bora basi taifa hilo katika kuzalisha mali na kukuza uchumi
ni ndoto.
Alibainisha
mfuko wa afya ya jamii CHF ni mkombozi wa wananchi ambao wako kwenye
sekta binafsi hivyo ni vyema jamii ikahamasika kujiunga nao.
Meneja huyo katika hatua nyingine alichangia kaya tano ambazo hawana uwezo na wako kwenye mazingira magumu ya kimaisha.
Aidha
meneja huyo alifanikisha kupata wanachama wapya katika kata hiyo ikiwa
ni jumla ya kaya 614 huku kaya wengine wakihamasika kujiunga na mfuko.
Adina
aliwashawishi wananchi hao kutumia fursa walizonazo ikiwemo tumbaku
kilo mbili tu zinatosha kujiunga na mfuko baada ya mauzo,jogoo na
biashara ndogo walizonazo kwani matibabu ni jambo zuri kwa afya zao na
kwamba ugonjwa unapokuja hautoi taarifa.
Aidha
alibainisha kuwa mwananchi yoyote ambaye atashawishi mwanachama
kujiunga na mfuko wa CHF atapewa kiasi cha sh 500 kama motisha ya
kusababisha mfuko kupata mwanachama mpya.kwa hisani ya http:.mjengwablog.com
Comments