Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Amri Kiemba amesema amekwenda Azam kufuata maslahi.
Kiemba alimwambia Mwandishi Wetu kuwa anaamini maisha popote, licha ya kukumbana na changamoto kadhaa.
Nyota huyo alisema ataitumikia Azam kwa juhudi zote iweze kutetea ubingwa wa Tanzania bara.
“Changamoto zipo, nivumilia mambo mengi Simba. Nimewahi kutuhumiwa
kuhujumu, mara kiwango kimeshuka kwa sababu ya umri mkubwa. Yote
nimekuwa na uvumilivu nayo,” alisema Kiemba.
Alisema anaamini kila mchezaji anataka maslahi, hivyo hakuona sababu ya kuacha kuichangamkia fursa ya kusajiliwa Azam FC.
Aliwataka mashabiki wa Azam kumpa ushirikiano ili kuiwezesha Azam
kupata mafanikio katika michuano ya Ligi Kuu na michuano ya Klabu Bingwa
mwakani.
Comments