Louis van Gaal hakufurahishwa na maoni ya Gary Neville baada ya mechi kumalizika.
Vita ya maneno baina ya Louis van Gaal na gwiji wa Man United Gary
Neville imeibuka kufuatia uchambuzi kuwa United ilibahatisha ushindi wa
2-1 dhidi ya Southampton.
Neville alidai United – iliyopo nafasi ya tatu Ligi Kuu baada ya
ushindi wa tano mfululizo – ilikimbia kifo baada ya ushindi wa magoli
mawili kutoka kwa Robin van Persie.
Gary Neville amesema mchezo wa Man U na Liverpool siku ya Jumapili utakuwa kama mchezo wa baa.
Mchambuzi huyo wa soka wa Sky alisema mechi ya United na Liverpool
siku ya Jumapili itakuwa “Mbwa na Bata dhidi ya Simba Mwekundu ila Van
Gaal mwenye hasira alisema: “Ni gwiji wa zamani, gwiji, mchezaji wa
zamani wa Man United, mauaji? Hayo ni maelezo ya Kiingereza – labda.
“Anaweza kusema chochote kwa sababu ni gwiji wa zamani, ila kama gwiji wa zamani, au kama gwiji, unapaswa kujua unachokisema.
“Unaweza kutafsiri upendavyo. Sio vigumu. Ninavyosema, anapaswa kuwa makini na maneno yake.”
Mlinzi wa kulia na nahodha wa zamani wa Man U Gary Neville amepewa jina la ‘gwiji wa zamani’ na kocha Louis van Gaal.
Pamoja na ukosoaji wa Van Gaal alikubali United ilipata bahati St Mary’s.
Neville aliyasema hayo kwenye Monday Night Football” “Sidhani (wanaweza kushinda ligi) hawana ubora huo.”
Comments