Roma inajiandaa kufanya uhamisho wa mlinda mlango wa
Chelsea,Petr Cech. Klabu hiyo ya Serie A inahisi atakuwa bora ndani ya
Italia na kuziba nafasi ya Morgan De Sanctis mwenye umri wa 38 ambaye
anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu.
Liverpool na Arsenal wanamtupia macho Andre-Pierre Gignac ili waweze
kupata saini yake ifikapo majira ya joto huku mkataba wa mfaransa huyo
ndani ya Marseille ukielekea ukingoni lakini wanakutana na upinzani
mkubwa jutoka kwa Dynamo Moscow ambayo imeonyesha pia kuvutiwa na nyota
huyo.
Mshambuliaji wa AC Milan,Nnamdi Oduamendi ameitaka klabu ya Crystal Palace imenyakue ili aweze kucheza Ligi Kuu ya Uingereza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Nigeria alifurahia
maisha yake kwa mkopo kwenye Serie B ambako Eagles walimpatia huko.
Southampton wanautupia macho usajili wa Januari kwa kutaka kupata
saini ya Bruno Martins Indi.Raia huyo wa Uholanzi alijiunga tu na Porto
kipindi kilichopita lakini meneja Ronald Koeman anataka kumnyakua ili
atue St Mary's.
Arsenal walituma maskauti kumtazama Marcelo Brozovic kwenye mchezo wa
sare ya 1-1 wa kuwania kufuzu kwa Euro 2016 baina ya Croatia dhidi ya
Italia .
Washika bunduki kwa muda mrefu wamekuwa wakivutiwa na kiungo huyo wa
Dinamo Zagreb na wapo tayari kutoa kaisi cha Euro milioni 6 ili kupata
saini yake.
Southampton wataitaka Tottenham kuwajumuisha nyota wake wawili ambao
ni Harry Kane na Andros Townsend kwenye dili lolote la kutaka kumnyakua
mshambuliaji Jay Rodriguez.
Liverpool wanajiamini juu ya kumsainisha mshambuliaji wa
Porto,Jackson Martinez. Wekundu hao wa Anfield wanamatumaini ya
kufanikisha dili la kumnasa kwa kiasi cha Euro milioni 37.7 pindi
dirisha la usajili litakapofunguliwa.
Mlinda mlango wa Tottenham,Hugo Lloris anatakiwa na Roma. Klabu hiyo
ya Serie A inahisi inaweza kumnasa raia huyo wa Ufaransa kwa kumpa ofa
ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Liverpool wanataka kuziba pengo la Glen Johnson kwa kumnasa Maxi
Pereira kutoka Benfica . Johnson amekuwa akihusishwa na kutaka kwenda
Roma wakati Pereira atakuwa nje ya mkataba ifikapo mwisho wa msimu.
Arsenal wanakutana na upinzani kutoka kwa Inter Milan juu ya kupata
saini ya kiungo wa Sevilla,Grzegorz Krychowiaking mwenye thamani ya Euro
milioni 30.
Raia huyo wa Poland alijiunga tu msimu uliopita lakini ameonyesha
ubora wa hali ya juu sana ndani ya Uhispania.Borussia Dortmund nao pia
wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo.
Comments