Rais wa Ukraine awaonya waasi Mashariki mwa nchi
Kaimu Rais wa Uraine, Oleksandr Turchynov,amewapa wapiganaji wanaounga mkono Urusi hadi mwisho wa leo Jumatatu kuondoka kutoka katika majengo ya serikali katika
miji ya mashariki mwa Nchi hiyo la sivyo wakabiliwe na jeshi la Ukraine wazalendo.
Bwana Turchynov amesema kuwa iwapo waasi hao hawatatii makataa hayo ya leo asubuhi, majeshi ya Ukraine yatatekeleza kile alichokitaja kuwa mashambulizi rasmi dhidi ya ugaidi.(MM)
Katika
hotuba ya runinga, rais huyo wa muda amesema kuwa hatokubali kuona
kilichofanyika Crimea mwezi uliopita kikirudiwa tena nchini mwake.
Huku hayo
yakijiri ,Urusi imelaani tahadhari hiyo ya Bwana Turchynov ,
ikiishutumu serikali ya Ukraine kwa kutangaza vita dhidhi ya watu wake .
Urusi
imepinga vikali tetesi za Marekani na Ukraine kuwa ndiyo inayochochea
ghasia hizo na uasi katika miji iliyoko mashariki mwa Ukraine .
Urusi
imesisitiza kuwa inataka kufanyike kwa mkutano wa dharura wa baraza la
usalama la umoja wa mataifa katika kipindi cha saa chache zijazo.
Rais wa Ukraine awaonya waasi Mashariki mwa nchi
Moscow imeomba umoja wa ulaya kuleta washirika wake walioko Ukraine kuwa chini ya udhibiti wake.
Ghasia na
taharuki imetanda kote katika miji iliyoko mashariki mwa Ukraine huku
waasi wakivamia majengo ya polisi na serikali wakiwa wamejihami kwa
silaha kali.
Wapiganaji wanaounga mkono Urusi, wengi wao waliokuwa wamejihami, wanaendelea kushikilia majengo ya serikali mjini Slaviansk .
Wanahabari
wa BBC waliokwenda Slaviansk, wamesema kwamba waasi wanaunga mkono
kujiunga na Urusi wamejenga vizuizi na kuasha moto barabarani usiku
kucha.
Picha za mtandao zaonesha ufyatulianaji risasi uliotokea wakati wa uvamizi huo wa vituo vya uma.
Afisa mmoja wa Ukraine anasemekana kupigwa risasi na kuuwawa.
Mjini Kharkiv, watu hamsini wamejeruhiwa huku makabiliano makali yakishuhudiwa katika mji wa Zapolrizhya.
CHANZO:BBC
Comments