Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Morogoro Mh Abdalah Shaweji Akisikiliza kwa Makini Taarifa za Chama cha
Mapinduzi alipowasili wilayani Mvomero kweny Maadhimisho ya Sherehe za
Siku ya Wazazi Mkoani Morogoro. Katibu wa Jumuiya Hiyo alifanya Shuguli
Mbalimbali Ikiwemo Kupanda miti Kufungua Mashina ya Chama cha Mapinduzi
Pamoja na Kukabishi kadi za Uwanachama ambapo Jumla ya Wanachama 150
walijiunga na umoja wa wazazi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Morogoro Mh Abdalah Shaweji Akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili Ofisi za CCM Wilaya ya Mvomero
Wajumbe wa Kmatai ya Utekelezaji wa
Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Wakisaini kitabu cha wageni kwenye
Ofisi za CCM Wilaya ya Mvomero.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Morogoro Mh Abdalah Shaweji aliyevaa Miwani Akipatiwa maelezo kuhusu
kilimo cha Mpunga kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mkindo kata ya Hembeti
Wilaya ya Mvomero ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Jumuiya ya wazazi .
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Morogoro Mh Abdalah Shaweji Akiwahutubia wananchi wa kata ya Hembeti
waliojitokeza kwa wingi katika Sherehe za Umoja wa wazazi Mkoa wa
Morogoro Ambapo katika Hotuba yake Aliwataka wana CCM Kushirikiana kwa
Pamoja Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa vitongoji na Vijiji.Pia
Alisisitiza Msimamo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro ni kwamba
Katika Katiba Mpya wanaunga Mkono Msimamo wa Chama cha Mapinduzi wa
Serikali Mbili na Kuwaomba wananchi Mara baada ya Rasimu ya Mwisho Kuja
waichague serikali Mbili katika Kura ya Maoni ya Kupitisha Katiba Mpya,.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Morogoro Mh Abdalah Shaweji Akipanda Miti katika Maazimisho ya
Sherehe za Jumuiya ya Wazazi
Wapenzi wa Chama cha Mapinduzi CCM
Kutoka Wilaya ya Mvomero wakiwa wamejitokeza kwa Wingi kwenye
Maadhimisho ya Siku ya umoja wa Wazazi Kimkoa ambayo Katibu wa Jumuiya
ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Mh Abdalah Shaweji Alikuwa Mgeni Rasmi kwa
niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo.
Wanachma wapya wa chama cha Mapinduzi wakiapa Mbele ya Mgeni Rasmi mara baada ya kukabidhiwa kadi.Inatoka kwa mdau.
Comments