Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa Mfuko unaosimamia mifuko ya hifadhi za Jamii nchini (SSRA)
, Irene Isaka ametoa wito kwa wanachama wapya kujiunga kwa wingi kwenye
mifuko hiyo kwa sababu muda si mrefu serikali itaweka uwiano wa mafao
sawa kwa mifuko yote.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa 32 wa
Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii (CISNA) wakiendelea na
Mkutano huo uliofunguliwa rasmi jana April 10, 2014 na Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Peter Ilomo (katikati mwenye tai nyekundu).
Isaka alisema hayo jana katika mkutano wa 32 ambao unazikutanisha nchi wanachama wa SADC unaendelea jijini Dar es Salam.
“ Tukiwa katika mkutano huu tunaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwa wenzetu wa SADC huku na
wao wakijifunza mambo kadhaa kutoka kwetu kwani zipo baadhi ya nchi
ambazo hazina mfuko mkuu kama SSRA ambao ndio mfuko mama unaosimamkia
kazi na utendaji wa mifuko mingine ya kijamii” alisema Isaka.
Aliongeza kwa kusema kuwa hivi sasa kumezuka mtindo kwa badhi ya mifuko
ya jamii kujipigia debe, hilo suala ni zuri ila jambo ambalo SSRA
tunapingana nalo ni la kunyang’anyana wanachama, hilo siyo jambo zuri
hata kama wako kibiashara,” alisema .
Aliongeza kwa kusema kuwa natoa wito kwa mifuko mbalimbali ya kijami
kuwa na ushindani endelevu wa kusaidia wanajamii ambao ndiyo wanachama
wao.
Aliongeza kwa kusema kwamba SSRA wakiwa wasimamizi wakuu wa mifuko ya
hifadhi za jamii wako katika mazungumzo na serikali kuhusu mifuko yote
iwe na kikokotoo kimoja kitakachoweka uwiano sawa.
Comments