Na Hudugu Ng'amilo Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba juzi usiku alikuwa miongoni mwa viongozi na watu mashuhuri waliotunukiwa nishani na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam. Katika maelezo ya kutoa nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano daraja la kwanza, ilielezwa kuwa Jaji Warioba, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuenzi na bado anauenzi Muungano huo. "Katika kipindi chako, pamoja na nyadhifa nyingine, ulikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani...katika kipindi hicho na hadi sasa umeendelea kuwa mwaminifu, umeutunza, umeulinda na umeuenzi Muungano," ilisema sehemu ya taarifa ya kutoa nishani. Hivi karibuni, Jaji Warioba amekuwa akishambuliwa na baadhi ya Wajumbe wa Bunge la Maalumu la Katiba, pia baadhi ya wana CCM kutokana na Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiong...