Skip to main content

Posts

Abaka, Awalawiti Watoto Akiwemo wa Kwake

Na Joseph Ngilisho, Arusha KATIKA hali isiyo ya kawaida baba mwenye familia, mke na watoto, David Samwel (21) mkaazi wa Moivaro, Nkwandua wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, anadaiwa kuwabaka na kuwalawiti watoto wanne wa kike wenye umri wa miaka 6 na 7, akiwemo mtoto wake wa kumzaa kwa nyakati tofauti chumbani kwake. Mtuhumiwa alitenda unyama huo kwa kumbaka pia mtoto wa mama mwenye nyumba wakati mkewe, akiwa ameenda kwenye biashara zake za kuuza mboga na kuwaacha watoto hao wakicheza nyumbani. Akisimulia mkasa huo, mama mwenye nyumba, (jina tunalihifadhi) mwenye umri wa miaka 30 alisema, aligundua mwanae (jina limehifadhiwa) amebakwa wakati alipotaka kumkosha. Alisema baada ya kumwita mtoto huyo, alikimbia na kwenda kujificha chumbani na alipomfuata aligoma kuvua nguo hali iliyomlazimu kumchapa ndipo alipomweleza alikuwa amefanyiwa mchezo mbaya na mtuhumiwa. Baada ya kumuangalia sehemu za siri aligundua alikuwa ameharibika vibaya na sehemu zake za...

Kenya: Al Qaida inatayarisha shambulizi Mombasa

Polisi ya Kenya imetahadharisha kuwa kundi la kigaidi la al Qaida linajitayarisha kufanya mashambulizi katika mji wa pwani wa Mombasa katika kumbukumbu ya mauaji ya msomi wa Kiislamu Sheikh Aboud Rogo. Taarifa ya polisi ya Kenya ambayo hadi sasa haijamtia nguvuni mtu aliyemuua msomi huyo wa Kiisalmu, imesema kuwa kundi la al Shabab linaloshirikiana na mtandano wa al Qaida, huenda linapanga kufanya mashambulizi ya kukumbuka kuuliwa msomi huyo. Mkuu wa polisi ya kaunti ya Mombasa Robert Kitur amesema jeshi la polisi limepata taarifa za kipelelezi kuhusu tishio la shambulizi la kundi la al Shabab katika mji wa Mombasa katika kumbukumbu ya mauaji ya Sheikh Aboud Rogo.  Kitur amesema usalama umeimarishwa zaidi katika mji wa Mombasa na kwamba polisi imezuiya maandamano ya kukumbuka tukio la kuuawa Sheikh Rogo. Waislamu wengi wa Kenya wanaituhumi serikali ya nchi hiyo kwamba ilihusika na mauaji ya Sheikh Aboud Rogo yaliyofanyika Agousti 27 mwaka jana. V...

Hii Syria !

Read more...

Miss Tanzania 2012 aanza ujenzi wa bweni la Albino Shinyanga

Brigette Alfred pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule ya msingi Buhangija wakinyanyua moja kati ya mabati 200 aliyonunua kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo,CHANZO:Majuto Omary. Na Mwandishi wetu, Shinyanga MREMBO wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija. Tayari mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 50. Makabidhiano hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Pet...

MCL sasa kuwajaza wasomaji mamilioni, magari matatu;

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imezindua promosheni kabambe ya 'Chomoka na Mwananchi' itakayowawezesha wasomaji wa gazeti la Mwananchi, kujishindia zawadi zenye thamani ya Sh250,000,000.Zawadi hizo ni pamoja na fedha taslimu na magari matatu mapya. Akizungumza katika uzinduzi huo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando, alisema promosheni hiyo itakayoanza leo, itafanyika nchini kote kwa siku 100 na kila siku kutakuwa na mshindi ambaye atajinyakulia Sh1,000,000. "Hii ni promosheni ambayo lengo lake ni kuwashukuru wasomaji wetu kwa kuendelea kulipenda gazeti lao na kuliweka juu hapa nchini," alisema Mhando. Alisema hadi mwisho wa promosheni hiyo (Novemba 30, mwaka huu), wasomaji 100 watakuwa wamejinyakulia fedha taslimu Sh100,000,000 na wengine watatu watapata magari mapya. "Lengo letu ni kuwawezesha wasomaji siyo tu kupata habari na kufikiri tofauti, bali pia kuweza kuwajenga kim...

Msome J Plus

Nyota huyo ambaye sinema zake zimeonekana kuwa na mapigano ya kutisha amefunguka kuwa kama kawaida yake yamo matukio yanayoambatana na matukio sahihi ya kipelelezi yanayovutia wadau kupatwa na hisia mara tu watakapoiona filamu hiyo. "Wadau wengi walikuwa wakiniuliza muendelezo wa sinema hii, napenda kuwatangazia kuwa siku si nyingi wataanza kuipata sinema hii,"alifunguka J Plus. Ndani ya ujio huo jamaa amemshirikisha mbambe mwingine wa filamu za mapigano Ibrahim Mbwana 'Bad Boy' pamoja na nyota kadhaa kama Charles Magari pamoja na Hashim Kambi na Veronica Viankero.

Msome Lulu

Bonyeza upate kumsikia .