Baraza la mawaziri nchini kenya limeamrisha mara moja afisi za serikali na taasisi za umma kuanza kupeperusha na kutumia bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kucheza wimbo wa Afrika Mashariki. Agizo hili pia linazihusu shule zote nchini humo. Nchini Tanzania, tayari kuna agizo kwamba Bendera ya Taifa inafaa kupeperushwa ikifuatiwa na Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, vivyo hivyo Wimbo wa Taifa utaanza kupigwa ukifuatiwa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mwandishi wa BBC David Wafula amezungumza na Waziri wa Utalii nchini Kenya Najib Balala ambaye alikuwa katika kamati iliyofanya uamuzi nchini Kenya na kwanza alimwuliza, umuhimu wa hatua hii ni upi?