WADAU wa mchezo wa soka hapa nchini wamewataka wachezaji wa timu ya taifa wacheze kwa kujituma ili wahakikishe wanaibuka na ushindi katika mchezo huo muhimu wa kuwania tiketi ya kufudhu kwa fainali za mataifa ya afrika za mwaka 2012.
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars jumamosi hii inatarajia kujitupa uwanjani kupambana na timu ya taifa ya Morocco mchezo unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza jijini Dar es salaam wadau hao wamesema ni dhahiri kwamba stars wana kazi ngumu ili waweze kupata ushindi katika mchezo huo huku wakiwataka kuweka kupigania taifa lao.
Stars katika mchezo wake wa kwanza na timu ya Taifa ya Argeria ikiwa ugenini ilitoka sare ya 1 – 1 na timu hiyo hivyo inailazimika kupata ushindi ili ijihakikishie nafasi ya kusonga mbele.
Stars inahitaji ushindi katika Mchezo huo wa kundi D ambalo lina timu za Argeria, Morocco, Tanzania na Afrika ya kati.
Comments