Bharti yatangaza mkakati wa kutoa huduma za kisasa kwa wateja Afrika
Kuingia ushirika wa kibiashara na IBM, Tech Mahindra na Spanco kuboresha huduma kwa wateja
Lagos, Nigeria – Oktoba 25, 2010 – Kufuatia ukuaji wa biashara barani Afrika na hata kukaribisha ushirikiano wa kibiashara baina ya wadau mbalimbali kwa lengo la kushiriki kuinua uchumi wa nchi mbalimbali, kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Bharti Airtel, imetangaza mpango wa ushirika wa kibiashara na kampuni za kimataifa za IBM, Techno Mahindra pamoja na Spanco ili kutimiza malengo ya kuinua huduma kwa wateja katika nchi za Afrika.
Makubaliano haya ambayo yanatarajiwa kukamilishwa hivi karibuni, Bharti Airtel, ambayo kwa sasa inamiliki na kuendesha biashara ya mawasiliano ya simu ya ‘Zain’ katika nchi 16 barani Afrika, itakabidhi makampuni hayo kuendesha vitengo vya huduma kwa wateja ukiwa ni mkakati madhubuti wa kukuza biashara katika eneo lote.
Kampuni hii ya mawasiliano ya simu, ambayo kwa sasa ina wateja takribani milioni 40 Afrika nzima, inatazamia kukuza idadi ya wateja hadi kufikia milioni 100 ifikapo mwaka 2013.
Kuteuliwa kwa washirika hawa wa kibiashara, IBM, Tech Mahindra pamoja na Spanco ambao wana uzoefu wa huduma zenye viwango vya kimataifa, kutawawezesha wateja wa Bharti Airtel kunufaika na huduma zenye viwango vya hali ya juu kabisa kwa kuwa washirika hawa tayari wanao uzoefu wa kuhudumia wateja katika ngazi za kimataifa hasa kwenye sekta ya mawasiliano, fesha na benki, bima na biashara za rejareja.
Pia, kwa Bharti Airtel kutangaza mpango huu wa ushirika katika biashara kwa nchi zote inazoendesha biashara ya mawasiliano barani Afrika, kutaleta manufaa thabiti katika maendeleo ya sekta ya mawasiliano kwa kila nchi husika, ikiwemo Tanzania. Hii ni pamoja na kuimarisha na kuongeza ufanisi na uwezo katika utendaji kazi pamoja na nyenzo husika.
Uendeshaji wa kitengo cha huduma kwa wateja, kwa hakika, kunabeba dhana muhimu katika kuifanya Bharti Airtel kuwa shindani zaidi barani Afrika, hususani wakati huu ambapo inatazamia kufanya huduma za mawasiliano kuwa nafuu zaidi na kuweza kupatikana kwa urahisi kwa kila mmoja katika soko la nchi zote 16.
Manoj Kohli, Afisa Mtendaji Mkuu (Kimataifa) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa pamoja wa Bharti Airtel amesema “Ushirika wetu na IBM, Tech Mahindra na Spanco unalenga kutazama upya na kasha kuboresha huduma zetu kwa wateja ili kufikia viwango vya kimataifa katika nchi zote 16. Kwa hakika hatua hii haitanufaisha tu wateja wetu, bali pia nchi husika mbamo tunaendesha biashara ya mawasiliano na hivyo kuchangia zaidi katika kuinua uchumi. Ushirika na kampuni zenye uzoefu wa kimataifa kama hizi ni chachu muhimu katika ukuaji wa sekta ya mawasiliano”.
“ushirika huu pia unatoa fursa ya kipekee katika kukuza ajira zaidi hasa kwa wafanyakazi wetu ambao wamejikita na kubobea katika kitengo cha huduma kwa wateja kwa vile inawafungulia milango ya kupata uzoefu zaidi kupiti kampuni za kimataifa zenye viwango bora vya huduma na teknolojia ya kisasa.” Alisema Kohli.
Hii ni mara ya pili kwa Bharti Airtel kutangaza ushirika na kampuni za kimataifa katika kuendesha biashara barani Afrika kwani mwezi Septemba makwa huu, iliiteua IBM kufunga na kuendesha mfumo wa teknohama kaika nchi zote 16.
”Uhusiano kati ya IBM na Bharti Airtel ni kudhirihisha malengo yetu katika kufikia masoko yanayokuwa kwa kasi duniani, ikiwemo Afrika”, alisema John Lutz, Mkuu wa Huduma za ushirikiano IBM.
Aidha, aliongeza kuwa “kitengo cha huduma za ushirika IBM husaidia wateja kuhimili vitengo vyake kama vile Huduma kwa Wateja kwa ufanisi zaidi na hata kuwafanya rasilimali zao nyingine katika maeneo mengine kama vile ukuzaji wa masoko, bidhaa na huduma husika”.
Kwa mujibu wa taarifa za utafiti zilizofanya na Deloitte kuhusiana na sekta ya mawasiliano, umiliki wa simu za mkononi barani Afrika ni chini ya asilimia 40. Hata hivyo, inaonyesha kuwa, kwa mujibu wa taarifa hiyo, mahitaji yamekuwa yakiongezeka kwa wastani wa asilimia 25 kila mwaka ilihali asilimia 10 pekee ya ongezeko inaweza kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea kwa nasilimia 1.2.
Vineet Nayyar, Makamu Mwenyekii wa Tech Mahindra amesema; “ni dhahiri kabisa ya kwamba kuna maeneo matatu makubwa ambayo Bharti Airtel itanufaika kutokana na kumilikisha kitengo chake cha huduma kwa wateja. Itakiza huduma zake kwa haraka wakati huo huo ikihimili mahitaji ya ukuaji, wateja watapata huduma za hali ya juu zenye kukidhi viwango vya kimataifa na wafanyakazi katika kila nchi watapata fursa ya kuboresha na kuendeleza taaluma zao.
“Kwa kuwa na ushirika wa makampuni haya matatu yenye huduma zenye viwango vya kimataifa ili kuboresha huduma barani Afrika, Bharti Airtel itaweza kuanza biashara yake kwa ufanisi madhubuti katika nchi zote. Kampuni zote tatu, kwa pamoja, zinato aajira kwa zaidi ya watu 90,000 katika huduma zake zinazotolewa kwa nchi ofauti 100 ilimwenguni kote.
Naye Kapil Puri, ambaye ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Spanco amesema: “Bharti Airtel amekuwa kinara katika ushirika wa kibiashara katika maeneo yake yote ya biashara huko India, Uzoefu na mafanikio iliyopata umesaidia umeisaidia nchi hiyo kuwa ni mfano bora ulimwenguni katika sekta ya ushirika wa kibiashara.
Takwimu za sasa zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 4000 wameajiriwa na Bharti Airtel kote barani Afrika, ikiwemo Tanzania, katika kitengo cha kuhudumia wateja. Hapo baadaye, inatarajiwa kuwa idadi ya waajiriwa katika kitengo cha kuhudumia wateja wa Bharti Airtel itaongezeka kutokana na mchakato wa kampuni ya Bharti Airtel kutanua mtandao wake wa mawasiliano na idadi ya wateja
Comments