Skip to main content

Posts

Showing posts from 2016

Wanaume watanashati vyuo vikuu watakiwa kujiunga kumsaka Mr.Handsome

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF) limesema kuwa  limeanza kuimiza wanafunzi wa vyo vikuu nchini kujiunga na kushiriki katika shindano la kumsaka Mr.Handsome . TBBF mara baada ya kuwa imezindua shindano hilo hivi karibuni hivi sasa  wanafunzi wanaotaka kujiunga kwa  kutumia mtandao wa www.tztbbf.org nakisha kubonyeza sehemu ya shindano kuchagua sehemu wanayotaka kushiriki. Akizungumzia hatua ya shindano hilo mmoja wa wasemaji wa shindano hilo Fike Wilson  alisema jana kuwa mara baada ya washiriki kuingia katika mtandao huo washiriki wanatakiwa kuandika jina kamili,Anuani , namba ya simu na anuani ya barua pepe. Alisema kama mshiriki atakuwa amefuata maelekezo hayo na kujiandikisha kwa ufasaha basi baadaya atapokea ujumbe  kwa njiaya barua pepe aliyoitoa hivyo washiriki wanatakiwa kuhakikisha wametoa anuani sahihi ya barua pepe. "Washiriki wakati wa kutumia parua pepe watatakiwa kuambatanisha...

KRC Genk yamfungashia virago Kocha wake

Boxing day yako imekujaje leo? basi kwa kocha Peter Maes imekua mbaya kwasababu kibarua chake kimeota nyasi kwenye club ya KRC Genk leo. Habari kutoka kwenye tovuti maalum ya club ya KRC Genk imetoa taarifa kuhusu kumaliza ushirikiano na kocha huyu baada ya kuanza kuifundisha club hii tangu msimu wa 2015/2016. Kocha huyu alianza majukumu ya kuifundisha club ya Genk mwaka 2015 hivyo basi ndiye kocha wa kwanza kumpokea Mbwana Samatta kwenye soka la Ulaya. Genk wamemtakia maisha mema kwenye majukumu yake mengine na maisha baada ya Genk.

Aliyechomwa Mkuki na Wafugaji Apata Nafuu Baada ya Mkuki Kutolewa

Maendeleo Ya Ndugu AUGUSTINO MTITU aliyejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki jana tarehe 25/12/2016 Kijiji cha Dodoma Isanga Kata Ya Masanze Jimbo La Mikumi na jamii ya wafugaji, hivi sasa anaendelea vizuri na matibabu baada ya kutolewa mkuki mdomoni salama salimini kwenye HOSPITALI YA MKOA MOROGORO na amelazwa wodi namba moja hospitalini hapo. Ofisi Ya Mbunge Jimbo La Mikumi inatoa shukrani zake za dhati kwa Madaktari na wauguzi waliofanikisha zoezi hilo, Lakini pia Ofisi Ya Mbunge Mikumi itakuwa ikiwapa maendeleo ya Bwana AUGUSTINO MTITU mpaka hapo hali yake itakapokua imetengemaa. Lakini la muhimu zaidi Mh. Mbunge amefanya mawasiliano na ngazi mbalimbali zinazohusika akiwemo Waziri wa Mambo Ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba juu ya kile kilichotokea na waziri amesikitika sana na ameahidi kulifuatilia suala hili kwa kina na kulitolea maamuzi magumu. Imetolewa na :- Robert A. Galamona Katibu Ofisi Ya Mbunge Jimbo La Mikumi

Solo Thang afunguka ya moyoni kuhusu Chidi Benz

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Solo Thang ameposti video akiwa na rapa Chidi Benz ambaye walikutana usiku na kuongea baadhi ya mambo, lakini kutokana na hali aliyokuwa nayo Chidi Benz Solo Thang alisema hawezi kumuhukumu bali anastahili kuombewa tu. Katika ujumbe ambao Solo Thang aliandika kwenye mtandao wake wa Instgram alisema hawezi kuhukumu na hata iweje bado Chidi Benz ataendelea kuwa mdogo wake, rafiki yake na mtu wake wa karibu. “Met with my Young brother Chid Benz last night almost cried, I dont judge, no matter what still my hommie, tumeongea sana, tuzidi kumuombea Mola” aliandika Solo Thang

Wanamitindo waonesha mavazi katika Sanaa Fashion Show

Jumamosi, lilifanyika onesho la mitindo la Sanaa Fashion Show kwenye viwanja vya kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Onesho hilo lililoandaliwa na mdau wa mitindo nchini, Shaksy liliambatana pamoja na utoaji tuzo kwa watu waliotoa mchango wao mkubwa kwa mwaka huu kwenye tasnia ya mitindo nchini na lilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo madisgner kibao akiwemo Asia Idarous, Martin Kadinda, Kulwa Mkwandule, Walter Dimaria, Agness, Alex na wengine wengi. Tazama picha zaidi hapa chini. Asia Idarous akimkabidhi G Tyga tuzo ya mwanamitindo bora 2016 Asia Idarous akimkabidhi Martin Kadinda tuzo ya Most Outstanding Male Designer 2016

Gereza kuu la Kigali lateketea kwa moto

Gereza kuu la Kigali maarufu 1930 Gereza kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia leo jioni moshi inaendelea kutanda. Kilichosababisha moto huo hakikajulikana. Shughuli za kuzima moto bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo. Hilo Ni gereza linalohifadhi wafungwa wa mchanganyiko wale wa kisiasa na wengine wa mauaji ya kimbari. Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa Ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka 4 iliyopita Kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia. Viongozi kadhaa serikalini wamefika kwenye eneo la tukio wakiwemo mawaziri na wakuu wa jeshi na polisi. Bado Ni mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa habari hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza kuu...

Rais Magufuli:Watanzania tuchape kazi kwelikweli

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo ambaye alikuwa chini ya malezi ya fundi seremala. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo (jana) katika Kanisa la Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu mjini Singida katika kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. “Katika kipindi cha maisha yake Yesu Kristo hapa duniani, mbali ya kwamba alizaliwa na mfanyakazi, Joseph seremala, lakini na yeye alishiriki katika kufanya kazi, basi niwaombe watanzania wote tuchape kazi kwelikweli kwa sababu hakuna cha bure,” alisema Rais Magufuli. Pia amewataka watanzania kuimarisha upendo, kuvumiliana, na kutobaguana, kwani upendo utalisaidia taifa kupata maendeleo huku akiwakumbusha waumini kuwa Yesu Kristo hakuwa CHADEMA wala CCM bali alikuwa ni wa watu wote. Rais Maguful...

Nyata Welbeck ameanza kufanya mazoezi vizuri

Baada ya miezi 7 ya kukaa nje ya kikosi kutokana na kupata maumivu ya kufundo cha mguu, hatimaye Welbeck ameanza kufanya mazoezi na kukimbia uwanjani. Striker huyu wa England na Arsenal alipata tatizo msimu uliopita mwezi wa tano kwenye mechi dhidi ya Manchester City na mechi kuisha kwa suluhu. Hijajulikana ni lini Danny atarudi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal lakini inategemewa mwanzo mwa mwaka 2017 anaweza kurudi akiwa amepona kamili kabisa kwa ajili ya mechi za Arsenal. Mwezi wa 10 manager Wenger alisema Welbeck yupo mbele zaidi ya mategemeo yao ya kupona kutokana na muda waliokadiria. Arsenal hawataki kumleta haraka mchezaji huyo uwanjani ili apone kamili kabisa. Danny alijiunga na Arsenal akitokea Manchester united mwaka 2014 akitoka Manchester united.

KOCHA AMSINI APEWA SHAVU RUVU SHOOTING

UONGOZI wa timu ya Maafande wa Ruvu Shooting umeingia makubaliano na Kocha Malale Hamsini kuifundisha timu hiyo kipindi cha mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom, Tanzania Bara. Kocha Malale tayari amewasili kambini Mabatini ambapo Jumatatu, Desemba 5, ataanza rasmi majukumu aliyokabidhiwa ya kukinoa kikosi hicho kama Kocha mkuu. Ofisa Habari wa wa Ruvu Shooting Masau Bwire alisema uongozi umefikia maamuzi ya kumchukua kocha huyo kutokana na uwezo wake mzuri wa kufundisha mpira kama unavyopambanuliwa na mafanikio makubwa katika timu alizowahi kuzifundisha. "Malale ni kocha mzuri sana, ameifundisha timu ya JKU kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuipandisha hadi ligi kuu ya Zanzibar mwaka 2013, msimu wa 2014 ikiwa mikononi mwake ilishika nafasi ya pili katika ligi hiyo ya Zanzibar, aliifikisha timu hiyo nusu fainali ya mashindano ya kombe la Mapinduzi, pia aliiwezesha kutwaa ubingwa wa mashindano ya majeshi mwaka 2013 Jijini Dar es salaam," al...

Ruge - Lady Jaydee wafikia patamu

Laydee amesema kauli aliyoitoa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kuhusu kuwa tayari kucheza nyimbo zake akiwaruhusu, ni sahihi na ya kiutuzima. Muimbaji huyo mkongwe ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano na mtangazaji wa Nyemo FM, ya Dodoma, Winston Makangale. “Nimeisikia kauli ya Ruge, kwa namna aliyoiongea na nafasi aliyokuwa nayo, sioni kama kuna kitu kibaya chochote alichokifanya kwa jinsi ambavyo amezungumza, naona amezungumza sahihi tu,” alisema. Amesema yeye na Ruge hawajahi kuzungumza kwa miaka minne sasa. “Hajanipigia simu na wala sijampigia simu, kwahiyo sio kwamba tumeongea kitu chochote lakini nayaona tu ni maamuzi ya kikubwa ambayo yamefanyika hapo. Hatujaongea kwasababu tulikuwa na mgogoro,” ameongeza

AZM FC INAJISUKA VEMA DIRISHA DOGO

Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM AZAM FC imemuacha mshambuliaji Muivory Coast, Ya Thomas Renaldo iliyemsajili mwanzoni msimu baada ya kusajili washambuliaji watatu kutoka Ghana.  Mapema mwezi huu, Azam FC iliwasaini washambuliaji Samuel Afful, Daniel Atta Agyei na Yahaya Mohammed wote kutoka Ghana. Na ili kubaki na wachezajin saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni, Azam imewatema Waivory Coast wote, beki Serge Wawa, kiungo Kipre Michael Balou na mshambuliaji Renardo walioingia timu hiyo kwa wakati tofauti. Balou alitangulia mwaka 2011 pamoja na pacha wake, Kipre Herman Tchetche ambaye mwanzoni mwa msimu alihamia Oman alikokwenda kujiunga na klabu ya Al Suwaiq, wakati Wawa alifuatia mwaka 2014, wakati Renaldo alisajiliwa Julai mwaka huu.   Afful, Agyei na Mohammed wanafanya idadi ya wachezaji wa Ghana kufika wane, baada ya beki Daniel Amoah aliyesajiliwa Agosti. Hao wanaungana na kiungo Jean Baptiste Mugiraneza kutoka Rwanda na Wazimbabwe wawli, winga B...

SPORTS ACADEMY YA KENYA WAIFUATA AZAM CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KITUO cha kukuza vipaji cha Green Sports Academy kutoka jijini Nairobi, Kenya kinatarajia kufanya ziara maalumu kwenye makao makuu ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC. Ziara hiyo ya siku sita itakayoambatana na mechi za kirafiki, itaaanza rasmi Desemba 20 jioni watakapowasili nchini hadi Desemba 25 mwaka huu watakaporejea nchini kwao. Green Sports itakuja nchini ikiwa na timu zake nne za umri tofauti chini ya miaka 13, 15, 18 na 21, ambapo itacheza mechi tatu za kirafiki kuanzia Desemba 22, 23 na 24 dhidi ya timu za vijana za Azam FC. Green Sports Academy ya Nairobi, Kenya inatarajiwa kufanya ziara maalumu Azam FC Uongozi wa kituo hicho kupitia kwa Mkurugenzi wa Ufundi, Stephen Ochiel Otieno, umetoa shukrani zake za dhati kwa uongozi wa Azam FC kwa kuwakubalia ziara hiyo ya kuja hapa nchini. Otieno amesema kuwa hiyo itawahamasisha sana vijana wadogo wenye vipaji kuelekea kuwa nyota wa kimataifa katika...

CRDB Yafunguka Kuhusu Tetesi ya Kuwa Imepata Hasara Kubwa Mwaka Huu

Benki ya CRDB imesema haijapata hasara kama tetesi zinavyoenezwa. Imesema kuwa imepata faida ya Bilioni 63 kwa kipindi cha Januari hadi Septemba, 2016. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Charles Kimei amesema mwaka huu wamepanga kufungua matawi 75 na kuajiri wafanyakazi 460. Dkt. Kimei amesema mwaka jana pekee wamefungua matawi 70 na kuajiri watu 450 jambo ambalo benki nyingi nchini haziwezi kufikia.

Mrisho Ngasa Kasaini Mbeya City

Picha inayo-trend kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni ya Mrisho Ngasa na afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten ambayo inaashiria tayari nyota huyo wa zamani wa Yanga ameshakamilisha deal na ‘wagonga nyundo wa Mbeya’ Mbeya City. Mwezi Septemba mwaka huu Ngasa alijiunga na Fanja FC inayoshiriki ligi kuu nchini Oman (Oman Professional League) ikiwa ni wiki tatu tu, baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya South Africa. Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Kagera Sugar, Yanga, Azam FC na Simba vyote vya VPL hajadumu Oman na hatimaye amerejea tena nchini na kusajiliwa na klabu ya Mbeya City ambapo ataungana na kocha wake wa zamani Kinna Phiri aliyemsajili kutoka Yanga kwenda Free State Stars kabla ya kocha huyo kutimuliwa kufatia mfululizo wa matokeo mabovu. Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten ame-post picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa pamoja na Mrisho Ngasa na kuandika maneno yanosomeka: “Mnapokamilisha jambo kutakiana heri ndio uung...

Kuanguka kwa Ndege ya Brazil Zatajwa, Mnusurika Aaanika Mazito!

Ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya mpira kutoka nchini Brazil ambayo ilipata ajali nchini Colombia inasemekana kwa muujibu wa taarifa zilizovuja ndege hiyo iliishiwa mafuta kutoka katika kifaa cha kurekodia mawasiliano. Katika mnara wa mawasiliano ya ndege, rubani alisikika akirudia mara kadhaa akiomba ruhusa ya kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya umeme iliyokuwamo ndegeni pamoja na kuishiwa mafuta ya ndege. Kabla hata mawasiliano hayo yaliyorekodiwa kufikia mwisho, rubani alisikika akisema yuko angani umbali wa futi elfu tisa sawa na mita elfu mbili mia saba na arobaini na tatu.Taarifa za mawasiliano hayo zimekuwa gumzo katika mitandao kadhaa nchini Colombia na hata katika vyombo vya habari nchini humo, na hivyo kumekuwepo fununu za taarifa hizo kuwa huenda zikawa na chembe ya ukweli kwamba kuishiwa kwa mafuta ndiyo chanzo zha ajali ya ndege hiyo. Wanajeshi wa Colombia waliliambia shirika la habari la AFP, kwamba pamoja na ndege hiyo ku...

Hatariii sijui ndio maendeleo mambo leo !!

: KIMENUKA:Cheki hapa uone picha alizoweka huyu mrembo ni aibumtupu My article last week was the first installment of a two-part series on how a senior can safely navigate the highly dysfunctional reverse mortgage market. I suggested that step one is to choose the combination of reverse mortgage features that best meets your needs, which can be done effectively using my HECM calculator, with or without the pro bono help of an expert. (See Selecting the Best Type of HECM Reverse Mortgage). Step two, discussed below, is to find the lender offering the best deal on the particular HECM you have selected. Read: Mother City housing project named best in SA Reverse Mortgages Have Two Lender Price Components: This is the interest rate and the origination fee. The tradeoff between them depends on how long you will have the mortgage — the longer you have it, the more important is the rate relative to the origination fee. My calculator does the work for you by showing how much...

Matumizi ya Smart Phone ni moja ya shida zinazoongezeka kwa jamii !!

IT'S VERY SAD....hapa ndipo tulipofikia. Juzi nipo katika gari mzee aliyekuwa na baskeli aligongwa AKIWA KATI YA BARABARA...Watu wanapiga PICHA huku wakitania...ATAKUWA AMEVUNJIKA KIUNO(mocking).. Huku wengine wakijipiga Selfie Badala ya Kumsaidia .....Very sad. You DON'T KNOW UR TOMORROW SIMU za Smart Phone Zimetufanya Tupoteza Ubinadamu.... IT'S VERY SAD....hapa ndipo tulipofikia. Juzi nipo katika gari mzee aliyekuwa na baskeli aligongwa AKIWA KATI YA BARABARA...Watu wanapiga PICHA huku wakitania...ATAKUWA AMEVUNJIKA KIUNO(mocking).. Huku wengine wakijipiga Selfie Badala ya Kumsaidia .....Very sad. You DON'T KNOW UR TOMORROW BUSU LA SHAVU LA MWIGIZAJI JULIA ROBERTS LAMDATISHA PAUL POGBA A+ A- Print Email BUSU la shavu kutoka kwa mwigizaji nyota wa Hollywood Julia Roberts limempagawisha kiungo wa Manchester United Paul Pogba ambaye ameposti picha yake na mwanamama huyo kwenye Instagram akiandaka na ujumbe "leo nimekuta...

Baada ya kusaini kwingine ..... Afunga ndoa

ABIDJAN, Ivory Coast BEKI wa zamani wa Azam FC, Serge Pascal Wawa amefunga ndoa na mzazi mwenzake aliyezaa nae watoto watatu. Wawa amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram picha zinazomuonyesha akiwa na mwanamke huyo katika nyuso za furaha huku akipokea salamu za pongezi toka kwa marafiki  kutoka sehemu mbalimbali duniani. Wawa amerejea kwenye timu yake ya zamani ya El-Merreikh ya Sudan baada ya kumaliza mkataba wake na matajiri wa Ligi Kuu ya Vodacom na hakutaka kuongeza mkataba kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokuwa na uhusiano mzuri na Kocha Mhispania, Zeben Hernandez. MANCHESTER UNITED YAICHAKAZA WEST HAM 4-1 NA KUCHUNGULIA KOMBE LA EFL ...Ibrahimovic, Martial moto chini, Schweinsteiger atoa gundu A+ A- Print Email MANCHESTER UNITED imeibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya West Ham katika mchezo wa robo fainali ya EFL Cup iliyochezwa Old Trafford. United itakutana na Hull City kwenye nusu fainali na iwapo itapenya basi itakuwa na kib...

WIZARA YA MAJI KUJENGA MTAMBO WA MAJITAKA UTAKAOGHARIMU BILIONI 200

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akitoa hotuba ya uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa kutathmini maendeleo ya sekta ya maji uliowashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa arnautoglo uliopo maeneo ya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa maendeleo wa sekta ya maji walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa kutathmini maendeleo ya sekta hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa arnautoglo uliopo maeneo ya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam. Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Wizara ya Maji na Umwagiliaji imejipanga kuanza ujenzi wa mtambo mkubwa wa majitaka katika maeneo ya Ilala Jijini Dar es Salaam ili kuzuia uchafuzi wa mazingira nchini. Hayo yamesemwa leo ...

Pep Guardiola:Awataka wachezaji kufanya tendo la ndoa na madem za

Samir Nasri alisema kitu ambacho kili make headline kubwa wiki hii kwamba manager Pep huwa anawambia wachezaji wafanye mapenzi kabla ya usiku wa manane ili wapate muda mrefu wa kupumzika. Nasri sasa hivi yupo kwenye mkopo Sevilla na hana dalili za kurudi City. Mambo mengine ambayo yapo wazi ni kwamba Pep alikata internet access kwenye eneo la mazoezi la Manchester City ili wachezaji waweze kuongea wao kwa wao na kuacha kutumia simu zao kwa muda mrefu. Kuhusu kufanya mapenzi mapema kabla ya usiku wa maneno sio kocha wa kwanza kuwa na imani hizo. Makocha wengi wanaamini kwamba kufanya tendo hilo mapema badala ya asubui humfanya mchezaji kuwa na nguvu za kutosha akiwa uwanjani. Kwenye mkutano wa waandishi wa habari bila kupoteza nafasi waandishi wa habari walimuuliza kocha Pep kuhusu maneno hayo ya Nasri. Jibu la Pep kuhusu yeye kuwaagiza wachezaji kufanya mapenzi mapema alijibu kwa mkato na kuendelea kuacha maswali mengi. Pep alisema, “Ni vigumu kwa mchezaji kuwa mch...

Arsene Wenger : Awatuliza Mzuka mashabiki atianeno hakuna kupanic

Manager wa Arsenal amewambia mashabiki wa club yake kwamba haina haja ya kupanic baada ya kutoa draw na wakiwa kwenye harakati za kumaliza juu ya group lao la UEFA. Manager Wenger alisema, “Haina haja ya kupanic kwasababu hatujapoteza mechi lakini tumepoteza kasi ya ushindi kidogo kwenye group letu. Nadhani tuna hali nzuri kwenye timu yetu. Kwa sasa hivi tuna asilimia 90 za kumaliza nafasi ya pili na hatujapoteza mechi yoyote. Itakua mbaya kutomaliza namba moja kwenye group letu?, sijui. Kitu kinachoniumiza ni kwamba tulitakiwa kushinda mechi lakini hatujashinda “. Mechi inayofuata ya Arsenal kwenye UEFA ni dhidi ya FC Basel ambayo itafanyika 6/12/2016 kwenye uwanja wa St Jakob Park huko Basel. Mechi iliyopita Arsenal walishinda kwa magoli 2-0 kwenye uwanja wa Emirates.

Upinzani DRC waanzisha kampeni ya "Kwaheri Kabila"

Zaidi ya vyama kumi vya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeungana kuanzisha kampeni ya kumshinikiza Rais Joseph Kabila kuondoka baada ya muda wake kukamilika mnamo tarehe 20 Disemba.Kampeni hiyo iliyopewa jina la "Kwaheri Kabila" inamtaka rais huyo anayeshutumiwa kwa kuchelewesha chaguzi, kuondoka madarakani bila ya masharti yoyote na kutangaza waziwazi kuwahatong'angania madaraka.SOMA ZAIDI; http://www.dw.com/sw

FA: Sioni Faida ya Kudandia Muziki Kama Singeli Wakati Naamini Aina ya Muziki Naoufanya.

Rapa Mkongwe Hamis ‘Mwana FA’ Mwin’juma, amefunguka na kusema kuwa anaamini aina ya muziki anaoufanya haoni sababu ya kudandia dandia aina ya miziki inayo ‘Trend’ kwa sasa ikiwemo Singeli.Akiongea kupitia kipindi cha Twenzetu cha Times Fm jana, FA amedai hana mamlaka ya kumkataza msanii yeyote kufanya aina ya muziki anayoitaka lakini kwa yeye hatoweza kufanya Singeli. “Kama mtu ameamua kurap juu ya mdundo wa Singeli mi ni nani hadi nimkataze? Kulikuwa na kipindi kila anayerap anataka kuimba, sio mbaya kwenda na Trend, mimi sifikirii kufanya Singeli nauamini sana mziki wangu” Alisema FA.Katika hatua nyingine rapa huyo amedai wimbo wake mpya wa ‘Dume Suruali’ ni muendelezo wa ‘Bado nipo nipo’ kwani yule bachela asiyetaka kuoa ameoa lakini hataki kuonga.

PRESHA ZA MASHABIKI SIMBA ZATULIA TSHABALAL AONGEZA MKATABA MPYA

Hatimaye uongozi wa Simba umewashusha presha mashabiki wake baada ya kumsainisha tena beki wake Mohamed Hussein Zimbwe kutokana na kuonesha umahiri katika kikosi cha kocha Joseph Omog. Zimbwe maarufu kama Tshabalala amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya makubaliano yaliyofanyika wiki moja na nusu iliyopita. Simba ilikubaliana na Zimbwe mbele ya baba yake mzazi na meneja wake, Herry Mzozo na leo ametia saini mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva. Tshabalala ambaye alishindwa kuaminiwa na Azam FC alifanya vizuri akiwa na Kagera Sugar kabla ya kusajiliwa na Simba ambapo kazi yake imeendelea kuonekana ndani ya klabu hiyo kongwe kwenye soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mkataba huo mpya kati ya Simba na Tshabalala sasa unakata kelele zote kuhusu nyota huyo kujiunga na klabu yoyote kat...

Dante awatiwa matumaini Yanga

MLINZI wa kati wa mabingwa wa Tanzania Yanga, Andrew Vicent 'Dante' amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa timu hiyo baada ya kuumia katika dakika za mwanzo za mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia hapo jana. Dante amesema leo  anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu jana huku akiamini anaweza kuanza mazoezi jumatatu hii kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam. "Nilipata maumivu makali nikaomba kutolewa, ila sasa sisikii maumivu kama jana, nitaanza mazoezi keshokutwa na Mungu akijalia nitakuwa tayari hata kwa mchezo wa Ngao ya Jamii na safari ya kuifuata Mazembe," alisema Dante. Beki huyo wa zamani wa Mtibwa  Sugar mwenye nguvu na anayetumia mbinu katika ukabaji amekuwa hapati nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza lakini mwenyewe anaamini ipo siku mwalimu atamwamini. "Niliumia sana roho kutoka jana, kiukweli nilipanga kuwaonyesha watu kile nilichonacho katika mechi kubwa kama ile. Lakini Mungu ndiye anajua, naamini siku ...

Wajua Umuhimu wa namba tisa

ZURICH, USWISI Anthony Martial (katikati) akifunga bao dhidi ya Liverpool, Clyne (kushoto) akisindika kwa macho KUNA washambuliaji wengi katika ulimwengu wa kandanda katika Ligi Kuu nchini Tanzania utakutana na namba tisa wengi kama John Bocco, Amis Tambwe, Donald Ngoma, Malimi Busungu na wengine wengi. Nje  ya Tanzania utawaona Michael Olunga (Kenya), Edin Dzeko (Bosni-Herzegovina), Luis Suarez (Uruguay), Clint Dempsey (Marekani), Mario Balotelli (Italia) na kadhalika. Mfano wetu utaanzia kwa nyota aliyekuwapo Liverpool ya England na sasa yupo katika klabu ya AC Milan huyo ni Mario Balotelli. Alipokuwa Liverpool wengi walikaririwa wakisema uwezo wa nyota huyo umekwisha hivyo kocha wake wakati huo Brendan Rodgers ikaonekana  alifanya usajili usio kuwa na macho akimwacha Luis Suarez atimkie Barcelona ya Hispania. Swali ni kweli Balotelli alikuwa akichezeshwa kama yeye alivyo au kocha Brendan alikuwa akimtengeneza kwa ajili ya nafasi  nyingine, ...