Samir
Nasri alisema kitu ambacho kili make headline kubwa wiki hii kwamba
manager Pep huwa anawambia wachezaji wafanye mapenzi kabla ya usiku wa
manane ili wapate muda mrefu wa kupumzika.
Nasri sasa hivi yupo kwenye mkopo Sevilla na hana dalili za kurudi
City. Mambo mengine ambayo yapo wazi ni kwamba Pep alikata internet
access kwenye eneo la mazoezi la Manchester City ili wachezaji waweze
kuongea wao kwa wao na kuacha kutumia simu zao kwa muda mrefu.
Kuhusu kufanya mapenzi mapema kabla ya usiku wa maneno sio kocha wa
kwanza kuwa na imani hizo. Makocha wengi wanaamini kwamba kufanya tendo
hilo mapema badala ya asubui humfanya mchezaji kuwa na nguvu za kutosha
akiwa uwanjani.
Kwenye mkutano wa waandishi wa habari bila kupoteza nafasi waandishi
wa habari walimuuliza kocha Pep kuhusu maneno hayo ya Nasri. Jibu la Pep
kuhusu yeye kuwaagiza wachezaji kufanya mapenzi mapema alijibu kwa
mkato na kuendelea kuacha maswali mengi.
Pep alisema,“Ni vigumu kwa mchezaji kuwa mchezaji mzuri uwanjani kama hafanyi mapenzi na mpenzi wake”. Pep alitoa maneno hayo akicheka na kuendelea na maswali mengine.
Comments