Manager
wa Arsenal amewambia mashabiki wa club yake kwamba haina haja ya
kupanic baada ya kutoa draw na wakiwa kwenye harakati za kumaliza juu ya
group lao la UEFA.
Manager Wenger alisema,“Haina haja ya kupanic kwasababu
hatujapoteza mechi lakini tumepoteza kasi ya ushindi kidogo kwenye group
letu. Nadhani tuna hali nzuri kwenye timu yetu. Kwa sasa hivi tuna
asilimia 90 za kumaliza nafasi ya pili na hatujapoteza mechi yoyote.
Itakua mbaya kutomaliza namba moja kwenye group letu?, sijui. Kitu
kinachoniumiza ni kwamba tulitakiwa kushinda mechi lakini hatujashinda
“.
Mechi inayofuata ya Arsenal kwenye UEFA ni dhidi ya FC Basel ambayo
itafanyika 6/12/2016 kwenye uwanja wa St Jakob Park huko Basel. Mechi
iliyopita Arsenal walishinda kwa magoli 2-0 kwenye uwanja wa Emirates.
Comments