Hatimaye
uongozi wa Simba umewashusha presha mashabiki wake baada ya kumsainisha
tena beki wake Mohamed Hussein Zimbwe kutokana na kuonesha umahiri
katika kikosi cha kocha Joseph Omog.
Zimbwe maarufu kama Tshabalala amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya makubaliano yaliyofanyika wiki moja na nusu iliyopita.
Simba
ilikubaliana na Zimbwe mbele ya baba yake mzazi na meneja wake, Herry
Mzozo na leo ametia saini mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva.
Tshabalala
ambaye alishindwa kuaminiwa na Azam FC alifanya vizuri akiwa na Kagera
Sugar kabla ya kusajiliwa na Simba ambapo kazi yake imeendelea kuonekana
ndani ya klabu hiyo kongwe kwenye soka la Tanzania na Afrika kwa
ujumla.
Mkataba
huo mpya kati ya Simba na Tshabalala sasa unakata kelele zote kuhusu
nyota huyo kujiunga na klabu yoyote katika kipindi hiki cha miaka miwili
bila kuvunja mkataba.
Comments