Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli, amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa
kwa Yesu Kristo ambaye alikuwa chini ya malezi ya fundi seremala.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo (jana) katika Kanisa la Parokia ya
Moyo Mtakatifu wa Yesu mjini Singida katika kuadhimisha Sikukuu ya
Krismasi ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
“Katika kipindi cha maisha yake Yesu Kristo hapa duniani, mbali ya
kwamba alizaliwa na mfanyakazi, Joseph seremala, lakini na yeye
alishiriki katika kufanya kazi, basi niwaombe watanzania wote tuchape
kazi kwelikweli kwa sababu hakuna cha bure,” alisema Rais Magufuli.
Pia amewataka watanzania kuimarisha upendo, kuvumiliana, na
kutobaguana, kwani upendo utalisaidia taifa kupata maendeleo huku
akiwakumbusha waumini kuwa Yesu Kristo hakuwa CHADEMA wala CCM bali
alikuwa ni wa watu wote.
Rais Magufuli ambaye aliambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli,
katika ibada hiyo amesema, kusali ni moja ya nguzo muhimu ambayo
Wakristo wote wanapaswa kutekeleza ili kuhakikisha taifa linaendelea
kubakia katika hali ya amani na utulivu ambayo ndiyo msingi wa
maendeleo.
Aidha, Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wakulima kote
nchini kuhakikisha wanazitumia vizuri mvua za sasa katika shughuli za
kilimo pamoja na kulima mazao yanayostahimili ukame.
Comments