Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF) limesema kuwa limeanza
kuimiza wanafunzi wa vyo vikuu nchini kujiunga na kushiriki katika shindano la
kumsaka Mr.Handsome .
TBBF mara baada ya kuwa imezindua shindano hilo hivi karibuni hivi sasa
wanafunzi wanaotaka kujiunga kwa kutumia mtandao wa www.tztbbf.org
nakisha kubonyeza sehemu ya shindano kuchagua sehemu wanayotaka
kushiriki.
Akizungumzia hatua ya shindano hilo mmoja wa wasemaji wa shindano hilo
Fike Wilson alisema jana kuwa mara baada ya washiriki kuingia katika mtandao
huo washiriki wanatakiwa kuandika jina kamili,Anuani , namba ya simu na
anuani ya barua pepe.
Alisema kama mshiriki atakuwa amefuata maelekezo hayo na kujiandikisha kwa
ufasaha basi baadaya atapokea ujumbe kwa njiaya barua pepe aliyoitoa hivyo
washiriki wanatakiwa kuhakikisha wametoa anuani sahihi ya barua pepe.
"Washiriki wakati wa kutumia parua pepe watatakiwa kuambatanisha walau si
chini ya picha nne na zisizidi saba wakiwa kwenye mikao tofauti wakat
watakapokuwa wanatumia kitufe cha kujiandikisha,"alisema Fike.
Fike alisema kuwa mshiriki atajiunga kwa kuingia katika mtandao wao
www.tztbbf.org kujiunga atalipia pesa ajili ya chahuo lake imwe ni shindano la
Mr.Handsome ,Mr.Photogenic au Mr .Tanzania kwani shindano lolote lile
atakalochagua atalipia kupitia tigo pesa , Mpesa aku kupitia benki kwa namba
na vielelezo vilivyo tolewa nakuwa mtumiaji atapokea namba na vielelezo
vilivyo tolewa.
Aidha alisema TBBF ikishirikiana na Pili Pili Entertainment LTD ndio
waandaaji wa mashindano ya Mr Tanzania kwa mwaka 2017 ambapo
mashindano ya Mr. Tanzania yatawakutanisha watunisha misuli wote wa
Taznania bara na visiwani pamoja kwa ajili ya shindano hilo lenye hadhi kubwa
nchini .
Pia alisema kilele cha fainali za mashindano haya kitafanyika siku ya june 30
mwakani 2017 jijini Dar es salaam , ambapo mshindi wa shindano la Mr.
Tanzania atawakilisha nchi kwenye mashindano ya Mr Africa , Mr Universe na
Mr World Novemba 2017.
Msemaji huyo ambaye pia yupo ndani ya dawati la ufundi la mchezo huo ,
alisema Kwa mara ya kwanza tangu kuazishwa kwa mashindano miaka ya tisini,
wajenga mwili watajiunga na kujiandkisha kupitia Gym na vilabu vya mazoezi
ya viungo tu kwa wanaoshindania taji la kimataifa la Mr. Tanzania.
Fike alisema uhamuzi huo umefanywa na kamati ya mashindano ya TBBF ili
kukuza na kuziwezesha utamaduni wa kufanya mazoezi ya Gym Tanzania.
Vigezo vya Mr Tanzania vitafanana vya vile vinavyotumika kwa Mr Afrika, Mr
World na Mr. Universe.
TBBF imesema imeanza kuingia katika vyo vikuu nchini katika kuwapa
maelezo wanafunzi wanaotaka kuwa Mr.Handsome ambapo tayari wao kama
waandaaji wameanza kugawa katika vio hivyo vipeperushi vinavyoonesha
namna ya kujionga shindano hilo.
Mwishoo.
Comments