Skip to main content

KOCHA AMSINI APEWA SHAVU RUVU SHOOTING



UONGOZI wa timu ya Maafande wa Ruvu Shooting umeingia makubaliano na Kocha Malale Hamsini kuifundisha timu hiyo kipindi cha mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom, Tanzania Bara.

Kocha Malale tayari amewasili kambini Mabatini ambapo Jumatatu, Desemba 5, ataanza rasmi majukumu aliyokabidhiwa ya kukinoa kikosi hicho kama Kocha mkuu.

Ofisa Habari wa wa Ruvu Shooting Masau Bwire alisema uongozi umefikia maamuzi ya kumchukua kocha huyo kutokana na uwezo wake mzuri wa kufundisha mpira kama unavyopambanuliwa na mafanikio makubwa katika timu alizowahi kuzifundisha.

"Malale ni kocha mzuri sana, ameifundisha timu ya JKU kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuipandisha hadi ligi kuu ya Zanzibar mwaka 2013, msimu wa 2014 ikiwa mikononi mwake ilishika nafasi ya pili katika ligi hiyo ya Zanzibar, aliifikisha timu hiyo nusu fainali ya mashindano ya kombe la Mapinduzi, pia aliiwezesha kutwaa ubingwa wa mashindano ya majeshi mwaka 2013 Jijini Dar es salaam," alisema Masau.

Mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, msimu wa 2015/16 alikwenda kuifundisha Ndanda FC ambayo ilimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ya msimu huo ikiwa ya pili kutoka mwisho lakini akaiwezesha timu hiyo kumaliza ligi ikiwa nafasi ya saba.

Aidha uongozi wa Ruvu Shooting ulisema kwamba, Malale akiwa na timu ya JKT Ruvu msimu huu wa ligi, mbali na timu hiyo kutokuwa katika nafasi nzuri ya msimamo ameiwezesha timu hiyo kuonesha ubora wa kucheza mpira wa kufundishwa.

"Tunaimani Malale ni kocha mzuri, kwa ushirikiano wake na msaidizi wake Seleman Mtungwe ambaye naye ni kocha bora mwenye viwango, timu yetu itakuwa imara na bora zaidi, itakuwa tishio na tutafanya vizuri mno katika msimu huu wa ligi" alisema Masau.

Malale ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, alianza rasmi kazi ya ukocha mwaka 2004 akiifundisha kwa mafanikio makubwa timu ya Ngome ya Fuoni na baadaye timu ya Faru ya Jumbi.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...