Skip to main content

Kuanguka kwa Ndege ya Brazil Zatajwa, Mnusurika Aaanika Mazito!


Ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya mpira kutoka nchini Brazil ambayo ilipata ajali nchini Colombia inasemekana kwa muujibu wa taarifa zilizovuja ndege hiyo iliishiwa mafuta kutoka katika kifaa cha kurekodia mawasiliano.

Katika mnara wa mawasiliano ya ndege, rubani alisikika akirudia mara kadhaa akiomba ruhusa ya kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya umeme iliyokuwamo ndegeni pamoja na kuishiwa mafuta ya ndege.

Kabla hata mawasiliano hayo yaliyorekodiwa kufikia mwisho, rubani alisikika akisema yuko angani umbali wa futi elfu tisa sawa na mita elfu mbili mia saba na arobaini na tatu.Taarifa za mawasiliano hayo zimekuwa gumzo katika mitandao kadhaa nchini Colombia na hata katika vyombo vya habari nchini humo, na hivyo kumekuwepo fununu za taarifa hizo kuwa huenda zikawa na chembe ya ukweli kwamba kuishiwa kwa mafuta ndiyo chanzo zha ajali ya ndege hiyo.


Wanajeshi wa Colombia waliliambia shirika la habari la AFP, kwamba pamoja na ndege hiyo kuanguka kuna shaka juu ya ajali hiyo kwani pamoja na ndege hiyo kuanguka hakukuwa na mlipuko wowote na kwamba huenda kulitumika nguvu ingine tofauti na nadharia ya kwisha kwa mafuta ndegeni.

Wadadisi wa mambo na wachunguzi bado hawako tayari kufungua mdomo na kuzungumzia juu ya chanzo chochote cha ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ya uchunguzi itatolewa baada ya miezi kadhaa.

Wachezaji wa timu ya Chapecoense walikuwa safarini kuelekea nchini Colombian kwenye mji wa Medellin mahali kulikotarajiwa mechi kubwa ya mpira wa miguu ya kihistoria na badala yake wachezaji hao wameacha historia .Kufuatia vifo vya wachezaji wa timu hiyo, ulimwengu mzima umeungana kuomboleza vifo vyao.kifaa-cha-ndege

Kwa muujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika shirika la ndege la Lamia watu wanne waliokuwa wasafiri na ndege hiyo wameponea chupuchupu kuwa miongoni mwa waliokufa baada ya kukosa tiketi.

Mmoja wa manusura wa ajali hiyo ambaye ni fundi wa ndege Erwin Tumiri, ameeleza namna alivyokwepa kifo, kwamba yeye alifuata maelekezo yote ya namna ya kujiokoa ,anasema abiria wenzie , walio wengi walisimama na kuanza kupiga kelele nay eye aliamua kuweka sanduku lake la kusafiria kati kati ya miguu yake na kuamua kubaki hivyo.

Visanduku viwili vya mawasiliano vya ndege hiyo vyote vilipatikana na tayari vimeanza kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa masuala ya anga.

Wachunguzi wataalamu kutoka nchini Uingereza wanasaidiana na mamlaka za Amerika Kusini kwasababu ndege iliyopata ajali ilitengenezwa na wana anga wa Uingereza BAE nchini Uingereza.Brazil imeanza siku tatu za maombolezo wakati maelfu ya watu na washabiki wa timu ya Chapecoense wako katika mji yaliko makao makuu ya timu hiyo Chapeco wanaendelea mkesha wa maombolezo wakati maandalizi ya kuchukua mabaki ya wachezaji hao inafanywa na jeshi kurejeshwa Brazil ili kuzikwa kwa pamoja katika uwanja wa Chapeco.

Nchi ya Bolivia tayari imekwisha tuma ndege ya kuchukua mabaki ya raia wake waliokufa katika ajali hiyo nchini Colombia.

Timu hiyo iliandika historia ya mafanikio katika soka kwa kuwa kileleni mwa ligi ya Brazil kwamara ya kwanza mwaka 2014.Kati ya watu 77 waliokuwa wameabiri ndege hiyo miongoni mwao ni watu sita tu ndiyo walionusurika .Abiria walio wengi walikuwa ni wachezaji wa timu ya Chapecoense na waandishi habari wapatao ishirini walikuwa miongoni mwa walipoteza maisha.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...